23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mwinyi aipongeza UN kuendea kuiunga mkono Zanzibar

Na Brighiter Masaki

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza Umoja wa Mataifa (UN), kwa azma yake ya kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi wake kupitia mashirika ya Umoja huo.
 
Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi alitoa pongezi hizo leo wakati alipofanya mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), nchini Tanzania Bwana Zlatan Milisic ambaye alifika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwa Rais.
 
Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi aliupongeza Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kutoa mashirikiano makubwa katika kuendeleza miradi kadhaa ya maendeleo ambayo ina tija kwa ustawi wa wananchi wa Zanzibar.
 
Rais Dk. Mwinyi alimueleza Mratibu huyo wa UN nchini Tanzania kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na juhudi zake za kuimarisha uchumi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi ikiwa imeweka kipaumbele katika utekelezaji wa mipango na Sera za Uchumi wa Buluu.
 
Rais Dk. Mwinyi katika mazungumzo yake hayo alieleza kuwa hali ya amani na utulivu ya Zanzibar imezidi kuimarika kutokana na mashirikiano mazuri yaliopo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo kipaumbele zaidi kilichowekwa hivi sasa ni kuhakikisha kunaimarishwa maendeleo endelevu.
 
Aliongeza kwamba kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kumeipelekea Zanzibar kuimarika kisiasa, kiuchumi na kijamii na kueleza matumaini yake makubwa ya kupata maendeleo zaidi kutokana na mashirikiano hayo yaliopo.
 
Alieleza kwamba kuibuka kwa maradhi ya COVID 19 duniani kupelekea sekta ya utalii kuzorota, sekta ambayo imekuwa ikitegemewa kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha pato la Taifa na uchumi wa Zanzibar.
 
Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi alimueleza Mratibu huyo wa UN, nchini Tanzania mikakati iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha uchumi wake huku akieleza matumaini yake kwa UN kuendelea kuiunga mkono Zanzibar kupitia mashirika yake makuu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles