Mwili ya Michael Jackson kufukuliwa

0
1569

NEWYORK, MAREKANI

TUHUMA za ulawiti zimeendelea kumwandama mfalme wa Pop duniani marehemu, Michael Jackson, baada ya mtandao wa RadarOnline kusema mwili wa staa huyo utafukuliwa kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Kupitia filamu ya Leaving Neverland imeelezwa kuwa Michael Jackson, aliwahi kuwanajisi wavulana zaidi ya 30 wenye umri mdogo ambao watatu tayari wamejitokeza kuzungumza.

Mmoja ya walalamikaji ni Wade Robson aliyethibitisha kwenye mitandao kuwa MJ alimlawiti toka ana umri wa miaka 7 hadi alipofika 14.

Mwingine ni James Safechuck jambo ambalo litasababisha mwili wa MJ kufukuliwa ili kupima vipimo vya DNA lengo likiwa ni kubaini kama kuna ukweli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here