20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Mwili wa mtu ambaye gari lake liliingia baharini waopolewa Mombasa

MOMBASA, KENYA

MWILI wa mtu ambaye gari lake liliingia baharini katika kivuko cha Likoni maarufu kama ‘Likoni Ferry’ jana saa nne na dakika 20 mjini Mombasa umeopolewa.

Polisi limemtaja mtu huyo kuwa ni John Mutinda mwenye umri wa miaka 46 na wakati mwili wake ukiopolewa kutoka baharini, mkewe Ruth Mueni alikuwa eneo la tukio.

Shirika la hudumu za Ferry nchini Kenya (KFS), limesema gari la John Mutinda lilishuka katika mteremko kwa kasi ya juu.

Kisa hicho kimerejesha upya kumbukumbu za mkasa mwingine wa mwezi Septemba mwaka huu ambapo Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu walikufa maji.

Iliwachuku waokoaji takriban siku 13 kuopoa miili  ya Mariamu na mwanae pamoja na gari walilozama nalo.

Taarifa ya KFS kuhusu kifo cha Mutinda ilisema: Dereva alikuwa akiendesha gari aina ya saloon ambayo namba zake za usajili hazijawekwa hadharani.

Kwamba baada ya kununua tiketi aliteremka kwa kasi katika mteremko wa feri na kuingia baharini.

Shirika hilo liliongezea kwamba dereva huyo alikataa kusimamisha gari hilo licha ya juhudi kadhaa za maafisa wa feri kumsimamisha.

Maboti ya uokoaji ya KFS, wanamaji wa Kenya  ‘Kenya Navy’ na maofisa wa polisi wakishirikiana na waokoaji wengine yalifika katika kivuko hicho mara moja na kuanzisha operesheni ya kulisaka gari hilo.

Gavana wa Mombasa, Hassan Joho mapema alikuwa amesema kwamba Serikali ya kaunti hiyo ilikuwa imepeleka kitengo chake kushirikiana na waokoaji wengine wa idara tofauti za Serikali.

KISA CHA MARIAM NA MWANAE 

Sept 29: Gari dogo aina ya soloon lililoarifiwa kuwa na watu wawili ndani lilizama katika kivuko cha Likoni

Sept 30: Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ferry, Bakari Gowa alisema wataalam wamebaini kuwa gari hilo lilizama kima cha mita 60, hivyo basi kufanya kuwa vigumu kuliokoa.

Sept 30: Shughuli za uokoaji ambazo zimejumuisha maafisa kutoka vitengo vya Kenya Navy, Kenya Ferry, na wapiga mbizi wa kibinafsi zilianza.

Okt 1: Kivuko cha feri kilifungwa kwa saa tatu ili kuruhusu utafutaji ulioendelea wa gari na miili ya waliokuwemo ndani.

Okt 2: Familia ya waathiriwa ililalamika kususua kwa  kwa operesheni ya uopoaji miili ya waathiriwa.

Okt 2: Kikosi cha pamoja katika operesheni ya uopoaji kilisema kimegunuda sehemu lilipo gari. Hii ni baada ya kuyakagua maeneo kadhaa yaliyoshukiwa kuwepo gari hilo.

Okt 3: Maofisa waliendelea kushughulika na ukaguzi wa maeneo yalioshukiwa kuwepo gari hilo.

Okt 7: Wapigambizi wa Afrika Kusini wajiunga katika operesheni hiyo ya uopoaji.

Okt 8: Wapigambizi walianza kazi ya kutafuta miili na gari.

Okt 9: Gari lililokuwa limezama katika kivuko cha Likoni lilionekana. Msemaji wa Serikali, Cyrus Oguna alisema haiwezi kuthibitishwa iwapo ndilo gari lililozama Jumapili Septemba 29.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles