25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Mwili wa Mengi kuwasili Jumatatu, kuzikwa Moshi Alhamisi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi unatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu Mei 5, ukitokea nchini Dubai kwa ndege ya Shirika la Emirates.

Dk. Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana Mei 2, nchini Dubai alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya kuwasili kwa mwili huo imetolewa leo Mei 3, na Mwanasheria na Msemaji wa familia ya Dk. Mengi, Michael Ngalo, alipokuwa akiwasomea taarifa ya ratiba ya mazishi waandishi wa habari jijinii Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo Ngalo, amesema mwili utakapowasili Jumatatu, utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, ambapo siku inayofuata Jumanne Mei 6, mwili utapelekwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar, kwa ajili ya kuagwa.

Aidha Ngalo amesema Jumatano Mei 7, mwili wa Dk. Mengi utasafirishwa kwenda Machame mkoani Kilimanjaro na anatarajiwa kuzikwa Alhamis Mei 8, ambapo ibada ya mazishi itafanyika katika kanisa la KKKT Kisereni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles