22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mwila asaidia ujenzi wa vyoo Yongwe, Kidugalo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chanika, William Mwila, ametoa msaada vifaa kuwezesha ujenzi wa vyoo katika Matawi ya Yongwe na Kidugalo yaliyopo kwenye kata hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Chanika, William Mwila (Wanne kulia), akikabidhi vifaa kwa Katibu wa CCM Tawi la Yongwe, Said Nyumba, kwa ajili ya ujenzi wa choo cha ofisi ya tawi hilo. Wengine ni wajumbe wa kamati ya siasa ya tawi hilo.

Msaada huo unajumuisha matofali 400, saruji mifuko 10 na masinki mawili ya choo.

Akizungumza Aprili 7, 2023 wakati wa kukabidhi msaada huo Mwila amesema ameguswa kusaidia ujenzi wa vyoo katika matawi hayo kwa lengo la kuhakikisha mazingira ya ofisi yanaboreshwa.

“Kitu unachoona kiko ndani ya uwezo wako kifanye kwa sababu chama ni chetu na lazima tukilinde, kila mtu atapimwa kulingana na kazi anazofanya hivyo, tufanye kwa vitendo. Niliahidi nitawezesha ujenzi wa vyoo na leo nimetekeleza ahadi yangu. Nawaomba tushirikiane sote kukamilisha ujenzi wa vyoo hivi,” amesema Mwila.

Aidha amewataka wanachama wa chama hicho kufanya kazi kwa bidi katika nafasi walizoomba na kuepuka kurithi maadui.

Naye Katibu wa CCM Tawi la Yongwe, Said Nyumba, ameshukuru kwa msaada huo akisema nia yao ni kuona chama kinasonga mbele siku zote.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Tawi la Kidugalo, Jaha Kalonda, amesema; “Vijana tujifunze kupitia kwa mwenyekiti wetu, aliahidi kwenye mkutano mkuu lakini hajasahau, ametekeleza ahadi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles