23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MWIJAGE AFICHUA SIRI KUFA VIWANDA TANGA

NA OSCAR ASSENGA-TANGA


WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,  amefichua siri ya kufa kwa viwanda nchini mkoani Tanga, kutokana na ushindani usio sawa hasa kwa bidhaa zinazoingizwa kwa njia ya magendo hali iliyosababisha kukosa masoko.

Amesema kitendo hicho cha kuingiza bidhaa kwa njia za magendo ni sawa na uhaini, ugaidi ambao unapaswa kushughulikiwa na wadau wote wa maendeleo ili kuweza kuutokomeza.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Tanga, wakati akifungua maonesho ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako na kuhusisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Alisema suala hilo linapaswa kuwekewa mipango mizuri ya kuhakikisha linatokomezwa ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ambayo itakuwa ni muhimili muhimu wa kufungua uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kufikia kipato cha dola 3000.

“Bidhaa nyingi zinaingizwa kwa njia ya magendo sana na hivyo kus+ababisha soko la bidhaa za ndani kushuka na huu ni sawa na uhaini na ugaidi kwa sababu bidhaa za magendo halizipiwi ushuru na madhara yake ni makubwa sana kwa ukuaji wa uchumi.

 “Kutokana na hilo niwaagize viongozi wa mkoa huu akiwemo RC (Mkuu wa Mkoa) na wakurugenzi kuhakikisha bidhaa za magendo haziingia nchini kwani madhara yake ni makubwa kwa Taifa,” alisema

Alisema madhara ya bidhaa za magendo inachangia kuua viwanda vya ndani na kuingiza sokoni bidhaa ambazo sio salama kwa matumizi.

“Kama tunazibiti magaidi wanaweza kuweka sumu kwenye biashara za magendo na zitakapowafikia watanzania watakula na kupoteza maisha hivyo hakikisheni mnapiga vita biashara za magendo na tumieni bidhaa zilizotibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS),” alisema Waziri Mwijage.

Awali akizungumza  katika kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella  alisema mkoa huo una utaratibu wa kujenga uhusiano kwa wananchi, wawekezaji na uwezeshaji kama moja ya eneo muhimu la kulinda na kukuza masoko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles