26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mwigulu: Ni ushamba kutumia mashangingi

Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amewashangaa baadhi ya watendaji wa serikali ambao wanapenda kutumia magari ya thamani kubwa (mashangingi) katika maeneo rahisi.

Mwigulu alisema Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kutokana na matumizi ya magari hayo na kueleza kuwa ni ushamba kwa watendaji hao kutumia magari hayo kwa maeneo kama Dar es Salaam.

Akizungumza jana asubuhi katika kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa na kituo cha televisheni cha TBC, Mwigulu alisema Serikali imekwishatafuta dawa kwa ajili ya kukabiliana na matumizi hayo.

Mwigulu pamoja na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, walialikwa katika kipindi hicho kwa ajili ya kuzungumzia Muswada wa Sheria ya Fedha, uliowasilishwa bungeni jana.

“Kwanza tumeamua kubadili utaratibu wa uagizaji wa magari, kwa sasa tutaagiza magari kwa pamoja lakini pia tunaachana na utaratibu wa kununua magari kutoka kwa dealers (wakala), magari yatanunuliwa kutoka kiwandani.

“Kwa muda mrefu watendaji wa taasisi na idara mbalimbali za serikali wamekuwa wakielekezwa wanunue magari madogo kama njia ya kudhibiti matumizi, lakini wamekuwa hawasikii.

“Tutakachofanya sasa ni kuwapelekea fedha za magari madogo, haina maana mkurugenzi atumie shangingi pale Dar es Salaam, ni ushamba ushamba tu huu unawasumbua watu,” alisema.

Mwigulu, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, alisema katika bajeti ya mwaka 2014/2015 fungu la magari serikalini limepigwa panga kwa asilimia 50, kutokana na utaratibu mpya wa uagizaji wa magari.

Akizungumzia muswada huo, Mwigulu alisema unalenga kuidhinisha matumizi ya serikali kwa mwaka huo wa fedha, baada ya bajeti kuu ya serikali kupitishwa.

Hata hivyo, Mwigulu aliwataka baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wenye tabia ya kukwepa kulipa kodi wakae chonjo, kwani amedhamiria kupambana na ‘mapapa’ hao.

“Katika sheria hii ndipo tunapofuta misamaha ya kodi, tumefanya hivyo ili kupata fedha, lakini pili kwa ajili ya kukuza uchumi, hapa tunaweka mazingira mazuri ya usimamizi wa fedha.

“Kwa muda mrefu mashirika ya umma wamekuwa wakijipangia bajeti zao na wanaleta asilimia 10. Sasa tutawalazimisha walete bajeti zao, walete tuzione.

“Wanakwenda kufanya semina Uingereza sijui Marekani tuwakatalie, hivi inakuwaje watu waende kufanya semina Marekani, kuna nini?

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles