32.3 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

MWIGULU: MLIOPEWA MADARAKA ACHENI KUONEA WANYONGE

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


                                                               

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mwigulu Nchemba amewaonya watu wenye madaraka waliopewa nguvu kisheria kuacha kuonea wanyonge na badala yake kutumia sheria hiyo katika kuwatetea.

Hayo aliyasema juzi wakati wa tamasha la Pasaka lililofanyika Dar es Salaam.

Mwigulu alisema hakuna hata siku moja uovu unaweza kuachwa na kuumiza wanyonge kwa masilahi ya wengi.

Alisema kila Mtanzania ana haki ya kuishi, hivyo ni vyema badala ya kuoneana kutumia muda huo katika kuliombea taifa ili liwe na amani sambamba na kumwombea Rais Dk. John Magufuli.

“Hata kama kuna mtu atatumia sheria katika kuonea wenziwe, hasa wanyonge kwa kufanya uovu, hawezi kuachwa akiendelea na mwenye nguvu kubwa hatakiwi kutumia kwa kuwaonea wanyonge, bali anatakiwa kutumia kwa kuwatetea wanyonge hao,’’ alisema Mwigulu.

Kuhusu nyumba za ibada, alisema ataweka masharti rahisi katika kuzisajili pamoja na taasisi zake kwa kuwa wizara yake ndiyo inayohusika na jukumu hilo ili mradi viongozi wa nyumba hizo wawe na uhuru wa kuabudu na si kuwakwaza watu wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles