24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MWIGULU AWAONYWA WANAOMBEZA RAIS  

 

Na PETER FABIAN


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amewataka watanzania kuunga mkono kwa dhati juhudi za Rais Dk John Magufuli katika mapambano dhidi ya vita ya  uchumi, rasilimali za taifa, ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma.

Kauli hiyo alitoa   Mwanza wakati akiwa mgeni rasmi katika hafla ya harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa kituo cha televisheni, radio na studio ya kurekodia cha Gombo  kusaidia kutangaza Injili cha Kanisa la EAGT Mwanza.

Kituo hicho  kiliasisiwa na Hayati Askofu Dk. Moses Kulola.

Nchemba ambaye ni Mbunge wa   Iramba Magharibi (CCM) aliwashauri  viongozi wa dini, watumishi wa Mungu na Watanzania wote waendelee kumuombea rais wakati huu akiwa kwenye mapambano hayo ya  uchumi, kutetea na kulinda rasilimali za taifa   ziweze kulinufaisha na kuwa na maendeleo.

Alisema  serikali ya Rais Magufuli imeanza kuwachukulia hatua mbalimbali kwa watuhumiwa wa ufisadi na wahujumu uchumi na inaendelea kuchukua hatua.

Waziri alisema   wapo baadhi ya watu na wanasiasa wamekuwa wakitumia maneno yenye viashiria vya uchochezi, kubeza na kumdhalilisha rais na serikali ya awamu ya tano kwa juhudi izinazochukuliwa kusimamia, kutetea na kulinda rasilimali za taifa kuwa watakutana na mkono wa sheria.

“Si kila kauli ni za siasa na maisha  ya watanzania hayana siasa hivyo ni vema kabla ya kuzitoa kauli hizo wazitafakari kama zina tija kwa wananchi.

“Hakuna siasa katika kulinda rasilimali zote za taifa bali ni jukumu la watanzania kuweka kando tofauti za itikadi na kushirikiana na serikali iliyopo madarakani kuzilinda,”alisisitiza.

Waziri   alisema   uchangiaji wa ujenzi huo utaendelea hadi kazi ya kukamilisha itakapofikia uzinduzi rasmi wa kituo hicho.

Alisema yeye na marafiki zake walichangia   Sh milioni 20 za kuanzia huku akiendesha mnada wa vitu ambavyo marehemu Askofu Kulola aliagiza kupigwa mnada kuchangia ujenzi huo.

Awali mtoto wa marehemu Askofu Kulola, Willy   Kulola ambaye ni mkurugenzi wa kituo hicho  alisema ziara ya  Waziri Nchemba ni kutekeleza maagizo ya marehemu baba yake Kulola.

Mjane wa marehemu Askofu Kulola, Elizabeth Kulola alisema   aliagizwa kumkabidhi vitu waziri huyo ili kusaidia kuvinadi na kuendesha harambee   kusaidia kufanikisha kukamilisha  ujenzi wa kituo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles