26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

MWIGULU AAGIZA BODABODA ZINAZOSHIKILIWA POLISI ZIACHIWE

Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuziachia pikipiki maarufu bodaboda zenye makosa madogo zinazoshikiliwa katika vituo vya polisi.

Mwigulu amesema hayo bungeni leo baada ya Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje (CCM) kuomba mwongozo wa Spika juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali kwa pikipiki zinazoshikiliwa katika vituo vya polisi nchini.

“Pamoja na kwamba pikipiki hizo zinashikiliwa kutokana na wamiliki wake kufanya makosa ya barabarani baadhi zinatakiwa kuachiwa ili wamiliki wake wakaendelee na shughuli za uzalishaji,” amesema.

Pamoja na agizo hilo, Waziri Mwigulu amesema pikipiki zilizokamatwa baada ya wamiliki wake kufanya makosa makubwa kama usafirishaji wa dawa za kulevya na ujambazi hazitaachiwa kutokana na uzito wa makosa ya wamiliki hao.

“Ili kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa, nitafuatilia kuanzia leo ili nione utekelezaji wake ulivyofanyika,” amesema Mwigulu.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyetaka baadhi ya pikipiki ziondolewe katika vituo vya polisi kwa kuwa ni nyingi sana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,560FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles