Safina Sarwatt, Moshi
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Kheri James anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake leo, Januari 13, mjini Moshi, Katibu wa (UV-CCM), Mkoa wa Kilimanjaro, Safina Nchimbi, amesema siku ya Januari 16 mwaka huu, James atazindua mradi wa nyumba ya makazi ya mtumishi wa UV-CCM, mkoa wa Kilimanjaro.
Aidha, siku ya Januari 17 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano la Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu mkoani humo ambalo litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa hapo.
“Yapo maelekezo ambayo aliyatoa Mwenyekiti wetu, Kheri James, ambayo aliagiza kwa UV-CCM nchi nzima, kuhakikisha kila wilaya na mkoa, anapofika kufanya kazi anataka kuona mtumishi ana mahali pazuri pa kuishi hivyo sisi kwetu mkoa wa Kilimanjaro tumetekeleza maagizo hayo.
“Hivyo, radi wa nyumba ya makazi ya mtumishi wa UV-CCM, umetekelezwa kwa nguvu za kujitolea kupitia kwa vijana wa UV-CCM na kuwapongeza kwa kuwa na moyo wa uzalendo wa kujitolea katika shughuli za ujenzi wa chama na taifa, hivyo tunamshukuru Mwenyekiti wetu kwa kutujali watumishi wake kwa kuhimiza kuwa na makazi bora ya kuishi,” amesema Safina.
Akizungumzia kongamano hilo, Nchimbi amesema litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa, ambapo litashirikisha mabaraza yote ya kata kutoka wilaya zote za Mkoa huo.
koa, sambamba na makada mbalimbali wa CCM wanaoishi mkoani humo, ambapo pia kongamano hilo litahusisha kuwaingiza wanachama wapya wa UVCCM, kuwapa mikakati, uwezo wa kutunza na kukitambua chama kinahitaji nini kwao,.
“Katika kongamano hili, mgeni rasmi atagawa vyeti vya shukrani kwa waliochangia ujenzi wa nyumba, ugawaji wa kadi kwa wanachama wapya, kutoa somo la Itikadi na Uenezi na kwamba kongamano hili litashirikisha makundi mbalimbali ya wasomi, viongozi wa dini, wanasiasa, viongozi wa Umma pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa huo,” amesema.