29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti TCCIA Pwani ahimiza wanachama kutumia fursa za viwanda

*Asema uwepo wa viwanda vingi umefungua fursa za masoko na ajira

Na Gustafu Haule, Pwani

MWENYEKITI wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Pwani, Said Mfinanga, amewataka wakulima kuhakikisha wanatumia kikamilifu fursa ya uwepo  wa viwanda katika Mkoa humo ili waweze kukuza kipato chao.

Mfinanga, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa TCCIA kutoka Wilaya za Mkoa wa Pwani kwenye mkutano mkuu wa Chemba hiyo uliofanyika Desemba 17, Mjini Kibaha.

Makamu wa Rais wa TCCIA anayeshughulikia viwanda, Clement Bocco akiwa katika mkutano Mkuu wa TCCIA Mkoa wa Pwani.

Amesema mkoa wa Pwani ni wa kimkakati wa viwanda na umebahatika kuwa na viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa mbalimbali zenye soko la nje na ndani.

Mfinanga amesema kuwa moja ya viwanda hivyo ni pamoja na kiwanda cha matunda cha Sayona Fruits kilichopo katika Kijiji cha Mboga katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo na viwanda vya usindikaji.

“Katika Mkoa wetu tunaviwanda vingi na sisi TCCIA tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatumia vizuri fursa hii lakini ninawaomba wanachama nao watumie fursa za viwanda vilivyopo katika maeneo yao kuzalisha kwa bidii kwakuwa masoko yapo,” amesema Mfinanga.

Mfinanga, amesema kuwa anaipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka kuboresha miundombinu mbalimbali kwa wawekezaji wa viwanda.

Amesema, awali kulikuwa na changamoto ya barabara, umeme na maji lakini kwa kiasi kikubwa changamoto hizo zimefanyiwa kazi kama mapungufu yapo katika maeneo machache na kwamba anaimani kuwa Serikali itaendelea kuyafanyiakazi mapungufu hayo.

Amewatoa wasiwasi wanachama wake kuwa TCCIA inafanyakazi vyema kwa kusimamia malengo yake ikiwemo kuboresha maslahi ya wanachama wake,kufanya utetezi wa masuala ya kibiashara,kutoa mafunzo ya kibiashara, kutoa ushauri kwa Wafanyabiashara kupashana habari za kibiashara na hata kutoa cheki kwa viwanda.

Kwa upande wake Makamu wa Rais upande wa Viwanda, Clement Bocco,amesema kuwa kazi kubwa inayofanyika ni kuhakikisha wanasimamia kikamilifu viwanda vinaanzishwa ili kutoa fursa kwa wananchama wao.

Bocco,amesema kuwa amefanya utafiti na kugundua kuwa wanachama wengi wanahitaji msaada wa karibu kutoka kwa viongozi wao hususani pale wanapotaka kuanzisha viwanda kwani mara nyingi wakuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Amesema changamoto hizo zinatokana na baadhi ya taasisi ambapo ameziomba taasisi hizo kuacha kuweka vikwazo pale mtu au mwanachama anapotaka kuanzisha kiwanda na kwamba wawatia moyo kwakuwa lengo ni kukuza uchumi wa nchi.

Mmoja wa wanachama wa TCCIA Mkoa wa Pwani kutoka Kerege Wilayani Bagamoyo ameipongeza TCCIA kwa kazi nzuri wanayofanya hasa katika kuwasaidia wanachama katika fursa mbalimbali za kibiashara.

Hata hivyo, Lihundi ambaye anamiliki kiwanda cha mafuta ya kupaka ametumia nafasi hiyo kuwaomba Wafanyabiashara wenzake hususani Wanawake kujiunga na TCCIA kwakuwa faida yake ni kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles