29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

MWENYEKITI SHIWATA AFARIKI

NA MWANDISHI WETU


MWENYEKITI wa Shirikisho la la Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib, amefariki dunia jana Jumamosi nyumbani kwake Ukonga jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Shaibu Taalib, baba yake alipatwa na umauti wakati akikimbizwa katika hospitali ya Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya shinikizo la damu yaliyokuwa yakimsumbua kwa kipindi kirefu.

Katibu mwenezi wa shirikisho hilo Peter Mwenda aliliambia Mtanzania kwamba, mazishi ya mwenyekiti wao yatafanyika leo nyumbani kwao mjini Bagamoyo.

Marehemu ndiye aliyeasisi shirikisho hilo na kufanikiwa kuanzisha kijiji cha wasanii kilichopo Mwanzega, Mkuranga mkoani Pwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles