29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti mpya CCM Nyamagana aanza na hili

Na Clara Matimo, Mtanzania Digital

Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Peter Begga amesema kwamba atafanya kazi kwa kushirikiana na wafanyakazi wote wa Halmashauri ya jiji la Mwanza lakini hatavumilia uongozi wa kinafiki ambao unakwamisha shughuli za maendeleo yanayofanywa na serikali.

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Costantine Sima (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao ambacho lengo lake lilikuwa ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Peter Begga(kushoto) kijitambulisha kwa watumishi wa halmashauri ya jiji la Mwanza(kulia ni Mkurugenzi wa jiji hilo Yahaya Sekiete.

 Begga ameyasema hayo Oktoba 25, 2022 wakati akijitambulisha  kwa wafanyakazi wa jiji la Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kuchanguliwa Oktoba Mosi mwaka huu katika nafasi hiyo.

Aliwaambia wafanyakazi hao kwamba wote ni wamoja maana wanamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa sababu wanafanya kazi kwa niaba ya serikali ambayo inaongozwa na CCM  kwa hiyo washirikiane kufanya kazi hasa wakizingatia kwamba wamezisomea na wao ndiyo wanaotatua changamoto mbalimbali za wananchi.

“Nyie mkifanya kazi vizuri na sisi chama tutafanya vizuri zaidi maana tumejipanga kuwahudumia watanzania na mimi sitapenda uenyekiti wa fitina fitina kuletewa majungu majungu kwamba fulani kafanya hivi kinafiki sitakubali tutaishi kirafiki na kwa kushirikiana lakini kazi iende ninachowasihi mfanye kazi kwa weledi kama mnavyojua CCM ndiyo msimamizi wa shughuli zote za maendeleo ambazo zinafanywa na serikali nchini na halmashauri ya jiji la Mwanza ikiwemo.

“Tukipata tatizo sehemu hatutakuwa watu wa kukurupuka na kuisema idara fulani hapana tutafuatilia kwa utaratibu maana tumejipanga  kuwahudumia wananchi kwa haki na kwa kutatua changamoto zao mimi kama mwenyekiti kijana siko tayari kuona ifikapo 2024 kwenye uchaguzi wa wenyeviti wa mtaa tunapoteza mtaa hata mmoja maana tukitatua changamoto za wananchi na wao wataendelea kukiamini chama cha Mapinduzi”alisema Begga na kuongeza.

“Utaratibu wa chama chetu cha Mapinduzi rais ni awamu mbili kwa hiyo wito wangu kwenu narudia tena ongezeni weledi mnapowahudumia wananchi ili itakapofika mwaka 2025 tukiwa tunamnadi mgombea wetu ambaye si mwingine bali ni Rais Samia Suluhu Hassan tusiwe na haja ya kujieleza wananchi wawe wameona mambo mazuri aliyowafanyia ambayo ndiyo dhamira yake ndiyo maana anaendelea kutafanya sisi wasaidizi wake ndani ya chama tutayasimamia na nyie wasaaididi wake upande wa serikali yatekelezeni vizuri,”alisema Begga.

Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya jiji la Mwanza wakiwa wanamsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Peter Begga(hayupo pichani) alipofika kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo lengo likiwa ni kuwataka washirikiane kutatua changamoto za wananchi.

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Yahaya Sekiete pamoja na Mstahiki Meya wa jiji hilo Costantine Sima walisema ushirikiano  uliopo baina ya CCCM na watumishi wa halmashauri hiyo ni mzuri huku wakimuahidi Mwenyekiti huyo kuendelea kushirikiana naye ili kuleta maendeleo na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020/2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles