23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti mpya bodi ya benki ya BOA Tanzania aanza kazi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Bodi ya BANK OF AFRICA TANZANIA, Dk. Nyamajeje Calleb Weggoro, ameanza kutekeleza mkakati wa kuendeleza benki kwa kutembelea matawi makubwa mawili.

Matawi aliyotembelea ni Business Center Oysterbay moja ya tawi ambalo ni kituo kikubwa cha kutoa huduma kwa wateja wa makampuni na biashara, na tawi la Victoria lililopo kijitonyama.

Ziara hiyo inakuja baada ya Dk. Weggoro kukutana na uongozi na wafanyakazi wa benki hiyo katika makao makuu ya benki hiyo yaliyopo jengo la NDC ambapo waliweza kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na kuboresha uendeshaji wa benki kwa ufanisi zaidi.

Mwenyekiti wa Bodi wa Bank of Africa  Dk. Nyamajeje Calleb Weggoro (Kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Wasia Mushi (katikati)  na Mkuu wa kitengo cha kuhudumia wateja wadogo Bw. Lomnyaki Saitabau wakati alipofanya ziara ya kikazi katika  tawi la Victoria jana.

Lengo la ziara ya Dk. Weggoro kwenye matawi hayo ilikuwa ni kuelewa shughuli za benki katika kusaidia maendeleo ya nchi na mchango wake katika kukuza ujumuishaji wa huduma za kifedha hususan kipindi hiki ambacho Tanzania imeingia katika uchumi wa kati.

Benki hiyo imeonekana kuwa thabiti katika kufanikisha uwekezaji uliofanywa nchini Tanzania na imeshiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo tangu 2007.

Pamoja na ushiriki wa benki hiyo katika miradi mbalimbali ya maendeleo, pia imeonyesha dhamira yake katika kusaidia biashara ndogo na za kati (SMEs) kwa kubuni bidhaa na huduma za kuvutia wateja.

Kama benki ya biashara, benki inayo wateja waliogawanywa katika makundi ya  wateja wa Rejareja, Biashara Ndogo na za Kati (SMEs) na wateja wa Makampuni.

Mwenyekiti wa Bodi wa Bank of Africa  Dk. Nyamajeje Calleb Weggoro (Kulia)  akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo,Wasia Mushi  wakati alipofanya ziara ya kikazi katika  tawi la Victoria jana

Kabla ya kujiunga na BOA-TANZANIA LIMITED, Dk. Weggoro, aliteuliwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kati ya mwaka 2016 hadi 2019 ambapo alifanya kazi kwa weledi mkubwa akisimamia maslahi ya nchi nane za Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Rwanda, Eritrea, Visiwa vya Shelisheli, na Sudan Kusini.

Dk Weggoro pia aliteuliwa kama Msaidizi na Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ushirikiano wa Kikanda na Masuala ya Uchumi), 2013-2016.

Mwenyekiti wa Bodi wa Bank of Africa  Dk. Nyamajeje Calleb Weggoro (kushoto) akiongea na Maofisa Waandamizi wa benki hiyo alipofanya ziara ya kikazi katika la Oysterbay  jana.

Kwa sasa anajiunga na timu ya BOA-TANZANIA kusaidia kuendeleza mipango na mikakati yake ya maendeleo na kuifikisha kwenye viwango vya juu kutokana na uzoefu na utaalamu wake mkubwa katika fani mbalimbali zikiwemo uongozi, uchumi, fedha, upangaji na utawala, uhandisi wa viwanda, upangaji wa miradi na kujengea uwezo tasisi.

Kwa njia nyingi Dk. Weggoro amehusika kuleta mabadiliko ya nchi mbalimbali za Kiafrika kupitia kushiriki kwake katika mipango ya maendeleo katika nchi alizowakilisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles