22.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Mwenyekiti Chadema Bariadi, wenzake wajiunga CCM

Derick Milton, Simiyu

Viongozi wawili na mwanachama mmoja wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakiongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo, Lazaro Singibala wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Viongozi hao wamepokelewa leo Jumapili Mei 31 na wanachama wa CCM Wilaya ya Bariadi wakiongozwa na Mwenyekiti wao Juliana Mahongo na Mkuu wa Wilaya hiyo Festo Kiswaga.

Wakizungumza mara baada ya kujiunga na CCM Singibala amesema kilichowasukuma kujiunga na CCM ni utendaji kazi mzuri wa Rais John Magufuli wa kuwaletea wananchi maendeleo.

Singibala amesema wakati akiwa Chadema kama kiongozi alikuwa na shauku ya kutaka kusifia baadhi ya kazi nzuri za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli lakini alishindwa kutokana na chama hicho kumkataza kufanya hivyo.

“Kuna kazi nzuri ambazo zimefanywa hapa Bariadi, nilitaka kumpongeza Rais Magufuli na viongozi wengine, lakini ukiwa Chadema ni marufuku kufanya hivyo hata kama ni kweli, ukiwa huko hakuna demokrasia, hakuna uhuru, wanataka kila kitu upinge hata kama ni kweli.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Bariadi na wenzake wawili wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha mapinduzi (CCM).

“Niliwaambia mtu akifanya vizuri tumpe haki yake, lakini wapi waligoma, kule hilo jambo la kupongeza halipo, niliona kwa nini niendelee kutesa moyo wangu, nikaona ni vyema kufanya maamuzi haya kujiunga CCM,” amesema Singibala.

Viongozi hao ambao wamejiunga na CCM ni Singibala ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, Buluda Mishono aliyekuwa mjumbe kamati tendaji Wilaya, na David Benjamini aliyekuwa mwanachama.

Mara baada ya kuwapokea wanachama hao, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Juliana Mahongo aliwapongeza kwa uamuzi huo wa busara, huku akiwakaribisha katika kukijenga chama na kuunga mkono juhudi za serikali za kuwaletea Watanzania maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,429FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles