25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti CCM Songwe akemea majungu ndani ya chama

Na Denis Sinkonde, Songwe

VIONGOZI na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ileje mkoani Songwe, wametakiwa kujenga ushirikiano na kuacha vitendo vya majungu na fitina ndani ya chama. 

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa CCM Mkoani wa Songwe, Radiwelo Tullo Mwampashi wakati wa Maadhimisho ya Miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika Februari Mosi, 2023 kiwilaya kata ya Kafule.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Radiwelo Mwampashi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Farida Mgomi.

Hfla hiyo iliambatana na shughuli za kijamii ikiwepo kupanda miti katika shule ya msingi Lupaso, kuwatembelea wagonjwa hospitali ya Isoko na kuwatembelea watoto yatima kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Isoko Orphans.

Mwampasi amesema katika kuenzi mchango wa waasisi ndani ya chama hicho viongozi ngazi ya mashina mpaka wilaya wahakiki wanachama hai na wasio hai ili kubaini makundi yanayopaswa kudhibitiwa kwa ajili ya kuondoa uhasama unaojitokeza kwa baadhi ya wana-CCM kudhorotesha jitihada zinazofanywa na Serikali.

Mwampashi amesema: “Ndugu zangu hiki chama kilianza siku nyingi viongozi wa chama tuache tabia hizi, ikiwemo za kukaa maofisini na kutaka kuabudiwa badala ya kutekeleza majukumu tuliyopewa.

“CCM ni chama ambacho kipo madarakani kwa miaka mingi tokea nchi hii ipate uhuru, mikononi mwa Baba wa TaifaHayati Mwalimu Julius Nyerere, hivyo mnapaswa kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa kwa mujibu wa katiba husika ili wananchi wasiweze kujengeka na dhana potofu,” amesema Mwampashi.

Aidha, Mwampashi amesema mifarakano au matatizo yoyote yale yanayojitokeza katika jamii, hayawezi kuleta amani bali hujenga chuki na kuondoa upendo miongoni mwao.

Katibu wa CCM wilayani humo, Hassan Lyamba katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama hicho amewataka wanachama wenzake kujiuliza wapi wametoka na wanakwenda wapi, huku wakiacha tabia za unafiki, uongo na fitina vitendo ambavyo kama wataviendekeza havitawafikisha mbali.

“Wewe kiongozi ukibainika unakisaliti chama, tutakushughulikia ipasavyo mpaka Yesu arudi duniani, hatutaki matendo ya ovyo ovyo na kusikia kila kukicha mnagombana,” amesema Lyamba.

Lyamba amefafanua kuwa Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wanaupendo, hivyo chama kilichopo madarakani hakitakubali kuiacha rehani kwa watu wabovu ambao hawana nia njema na taifa hili.

Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo, Diana Ngabo amewaasa wanachama wa CCM wa wilaya hiyo kwamba wawabeze watu ambao wakati wote wamekuwa na tabia ya kupinga maendeleo pale yanapofanyika.

Wilaya ya Ileje imeadhimisha kuzaliwa kwa CCM kiwilaya katika kata ya Kafule kitongoji cha Kagwina huku mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles