26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

MWENGE WAZUA KIZAAZAZA BUNGENI

Na MWANDISHI WETU-DODOMA


MBUNGE wa Viti Maalumu, Rhoda Kunchela (Chadema), amehoji hatua ya wafanyabiashara na wafanyakazi kulazimishwa kuchangia fedha za mbio za Mwenge.

Alihoji hayo bungeni jana, alipokuwa akiomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge.

“Mheshimiwa mwenyekiti, hapa nilipo nina risiti (stakabadhi) kama 300 zinazoonyesha walimu, wafanyabiashara na wafanyakazi wengine nchini, wanavyolazimishwa kuchangia fedha za Mwenge.

“Kwa nini inakuwa hivyo wakati Serikali ilishaeleza kuchangia Mwenge siyo lazima bali ni hiari? Kwa hiyo, naomba mwongozo wako juu ya hili na ikibidi Bunge lisitishe shughuli zake ili lijadili jambo hili,” alisema Kunchela.

Akijibu mwongozo huo, Chenge alimtaka mbunge huyo awasilishe stakabadhi hizo serikalini ili zikafanyiwe kazi.

“Nakuomba upeleke hizo risiti zako serikalini wakazifanyie kazi, lakini hilo suala la kutaka Bunge lisitishe shughuli zake kwa ajili ya kujadili suala hilo, haiwezekani kwa sababu hata kanuni ya 68 (7) uliyotumia kuwasilisha hoja yako, haitoi nafasi hiyo kwa jambo ambalo halikutokea hapa bungeni hivi punde,” alisema Chenge.

Wakati huo huo, Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Ditopile (CCM), alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2017/18 iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki na Waziri Dk. Charles Tizeba, aliitaka Serikali ijikite katika tafiti kwa kuwa zinasaidia kukuza sekta ya kilimo.

Katika mchango wake, mbunge huyo alizitolea mfano nchi za Uganda na Malawi ambako pamba inalimwa kwa mafanikio zaidi baada ya kufanyika utafiti wa kutosha.

Kwa upande wake, Mbunge wa Igalula, Mussa Ntimizi (CCM), alilalamikia mazingira mabovu ya ufugaji, kwa kuwa maeneo mengi yanayofaa kwa ufugaji yamechukuliwa na Serikali na kufanya hifadhi za yaifa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,922FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles