26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Mwenge wazindua kampeni Binti Shujaa Handeni

Amina Omari, Handeni

Mwenge wa Uhuru jana umezindua kampeni ya Binti Shujaa, ambayo itashughulikia  kumaliza tatizo la mimba na ndoa za utotoni na kuboresha mazingira ya usafi kwa mtoto wa kike wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kampeni hiyo pia imelenga katika ugawaji wa taulo za kike bure kwa wasichana zaidi ya 2,000  kuanzia shule za msingi na kuweka miundombinu ya maji na vyoo katika hali ya usafi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema kuanzishwa kwa kampeni hiyo ni mmoja ya ndoto zake za kukomesha mimba za utotoni wilayani humo.

“Ndoto yangu ni kuona watoto wa kike ndani ya wilaya hii wanapata fursa ya kupata elimu bila vikwazo vyovyote na kuwachukulia hatua kali wale watakaobainika kuwapa mimba na kuwaozesha mabinti,” amesema Gondwe.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ally, amezitaka taasisi zinazojishughulisha na utetezi wa watoto kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu mashauri yanayohusu watoto.

“Hakikisheni kesi za manyanyaso dhidi ya watoto zinapokuja katika madawati yenu mnaziamua kwa mujibu wa Sheria badala ya kumalizana kifamilia,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles