29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenge wa Uhuru wapokelewa Nyamagana Jiji la Mwanza

*Kumlika miradi yenye thamani zaidi ya Sh bilioni 5.6

Na Clara Matimo, Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza , Amina Makilagi, leo Julai 17, 2022 saa 3:30 asubuhi  amepokea   Mwenge wa Uhuru katika  eneo la Kamanga ferry ukitokea Wilayani  Ukerewe  Mkoani humo  huku  akibainisha kwamba utakimbizwa  katika kata sita kilomita 24.2.

Viongozi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza wakiulaki na kushika Mwenge wa Uhuru ulipowasili jijini humo mapema leo.

 Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi waliofurika katika eneo hilo kuulaki Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Kanali Denis Mwila, Makilagi amesema ukiwa wilayani humo utazindua miradi mitatu utafungua miwili pia utaweka jiwe la msingi katika mradi mmoja yote ikiwa na thamani ya Sh bilioni 5,617,850,358.

“Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela ikiwemo ya elimu, barabara, maji na afya, miradi tunayoitekeleza ni mingi lakini Mwenge wa Uhuru  utaifikia miradi sita  kati ya hiyo  miwili itazinduliwa, miwili itafunguliwa na mmoja utawekewa jiwe la msingi.

“Miradi itakayozinduliwa ni mradi wa mfumo rahisi wa maji taka kwenye makazi ya miinuko uliopo Kata ya Igogo uliotekelezwa kwa thamani ya Sh bilioni 3,844,768,483, jengo la benki ya CRDB Tawi la Buhongwa Sh milioni 500 na mradi wa Youth Box Media House uliogharimu Sh milioni 81,” amesema  Mkuu huyo wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza na kuongeza

“Miradi itakayofunguliwa ni ujenzi wa barabara za Hessawa Yatch makaburini (420) na  Tilapia- Vick fish (230) iliyojengwa kwa kiwango cha lami kwa thamani ya Sh milioni 345,798,653 na ujenzi wa vyumba sita vya madarasa shule ya sekondari Mkuyuni  uliogharimu Shmilioni  328,283,222,”amefafanua Makilagi.

Aidha ameutaja mradi mmoja ambao utawekewa jiwe la msingi kuwa ni ujenzi wa miundombinu katika kituo cha afya Bulale ambacho kipo Kata ya Buhongwa huku akifafanua kwamba  umegharimu Sh milioni 500.

Awali akiongea katika viwanja hivyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, 2022, Sahili Geraruma amesema “Halmashauri zote ambazo zimekwishapitiwa na Mwenge wa Uhuru zizingatie maelekezo yote yaliyotolewa na Mwenge wa Uhuru ili kuboresha miradi ya maendeleo inayotekelezwa na fedha za Serikali katika maeneo hayo.

“Sambamba na hilo tunaomba tukute taarifa za miradi ndani ya magari yetu na nyaraka original maeneo ya miradi pamoja na wataalamu waliopewa dhamana ya usimamizi wa miradi hiyo,”amesema Geraruma.

Geraruma aliwaelimisha na kuwahamasisha wananchi wa jiji la Mwanza kama alivyofanya katika halmashauri zote ambazo Mwenge wa Uhuru umekwishapita umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ili kuiwezesha Serikali  kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo ya watu wake katika sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu, hali ya ajira, nishati maji safi na miundombinu kama barabara.

Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa, 2022 inasema ‘Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo Shiriki Kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo ya Taifa’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles