Na Clara Matimo, Mwanza
Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo Julai 19, 2022 katika Halmashuri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ukitokea Halmashauri ya Buchosa wilayani humo.
Makabidhiano ya Mwenge huo yamefamywa baina ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Buchosa, Julius Mulongo na wa Sengerema Binuru Shekidele, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Bungonya Kata ya Nyamazobe.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga, amesema kwamba ukiwa wilayani humo, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilomita 91.1, utaipitia miradi mitano yenye thamani ya Sh bilioni 1.3 kati ya miradi hiyo mitatu itazinduliwa na miwili itawekewa mawe ya msingi.
Kwa mujibu wa Ngaga miradi itakayozinduliwa ni vyumba sita vya madarasa Shule ya Sekondari Katunguru, mradi wa kikundi cha vijana cha Tujiinue wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki na kilimo cha bustani katika Kijiji cha Mayuya poja na kituo cha kuuzia mafuta cha SIlya kilichopo Bukara.
Ngaga ameitaja miradi itakayowekewa mawe ya msingi kuwa ni wa maji ya bomba Nyamililo na jengo la dharura katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.
Baada ya kukimbizwa katika halmashauzi zote nane Mkoani Mwanza Mwenge wa Uhuru unatarajia kukamilisha mbio zake mkoani humo kesho Julai 20,2022 kuanzia saa 2:30 hadi 3:30 katika eneo la Kasamwa ambapo Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel, atamkabidhi Mkuu wa Mkoa ya Geita Rosemary Senyamule.