28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mwenge wa Uhuru waanza mbio zake Simiyu

Na Derick Milton, Busega

Mwenge maalumu Uhuru 2021 umeanza mbio zake leo Jumatatu Juni 28, 2021 katika Mkoa wa Simiyu, ukitokea katika mkoa wa Mara ambapo ukiwa mkoani humo unatarajia kukimbizwa kwa siku tano katika Wilaya za Busega, Bariadi, Itilima, Meatu pamoja na Maswa.

Akipokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Mara, Ally Happi mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila amesema kuwa mwenge ukiwa mkoani humo utaweka jiwe la msingi, kufungua, kuzindua, kuona jumla ya miradi 40.

Kafulila ameongeza kuwa miradi hiyo yenye thamani ya Sh bilioni 14.9 ipo katika sekta ya Tehama, Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Barabara, Mazingira, Viwanda, Utawala, Maendeleo ya jamii, pamoja na Sekta binafsi.

“Mwenye maalumu wa uhuru mwak 2021, mbali na kuzindua, kuona na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi mbalimbali, utapata nafasi ya kuangalia miradi ya mwaka 2019 ili kuangalia jinsi inavyoendelea kutoa huduma kwa wananchi,” amesema Kafulila.

Akizungumzia juu ya ujumbe wa mwenge mwaka huu kwenye suala la lishe bora kwa afya imara, Kafulila amesema mkoa huo umeweka mikakati ya kuhakikisha unapunguza idadi ya watoto chini ya miaka mitano wenye udumavu na ukondefu kwa kiwango kikubwa.

Akisisitiza kuhusu udumavu amesema mkakati uliopo ambao unatekelezwa na mkoa kwa kushirikiana na wadau wengine, ni kupunguza asilimia ya watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 31.2 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 15.6 mwaka 2025.

“Aidha, kama mkoa tunao mkakati mwingine wa kupambana na tatizo la ukondefu kwa watoto chini ya miaka mitano, kutoka asilimia 4.6 mwaka 2020, hadi kufikia asilimia 2.3 mwaka 2025,” amesema Kafulila.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge, Luten Josephine Mwambashi, akitoa ujumbe wa mwenge kwa wananchi wa Mji wa Lamadi amewataka kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na rushwa pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya kwa vijana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles