24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenge kuzindua miradi 64 Tanga

Amina Omari, Korogwe

Mkoa wa Tanga umeupokea Mwenge wa Uhuru huku ukitarajiwa kuzindua miradi 64 yenye thamani ya Sh bilioni 126.4.

Akiupokea mwenge huo uliotokea mkoani Kilimanjaro jana, Mkuu wa mkoa huo, Martine Shigela mbali na miradi hiyo pia mwenge huo utakagua, kufungua, kuzindua pamoja na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali iliyoko kwenye halmashauri 11 za mkoa huo.

“Miradi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano uliopo baina ya serikali, wananchi pamoja na washirika wa maendeleo na ujumbe wa mwenge mwaka huu umelenga katika kuimarisha huduma za maji vijiji na mijini,” amesema.

Amesema Mkoa wa Tanga umefanikiwa kutumia kiasi cha Sh bilioni 12 katika kukamilisha miradi ya maji katika maeneo mbalimbali.

Aidha, amesema ili kufikia wastani wa kitaifa wa asilimia 72, mkoa umejipanga kuelekeza nguvu katika miradi michache yenye kuleta matokeo ya haraka.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ally amewataka wananchi kuhakikisha wanashiriki katika miradi ya maendeleo na kuilinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles