30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mwenge kuzindua miradi 44 Manyara

Na BEATRICE MOSSES

-MANYARA 

MWENGE wa Uhuru umewasili mkoani hapa na unatarajiwa kuzindua miradi 44 iliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 8 katika halmashauri saba. 

Miradi hiyo ipo katika halmashauri za Mbulu Mji, Wilaya ya Mbulu, Hanang, Babati Mji, Babati, Kiteto na Simanjiro. 

Akipokea Mwenge huo ukitokea Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, alisema kati ya miradi 44 inayotarajiwa kuzinduliwa, 16 itawekwa jiwe la msingi.

Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Manyara, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkongee Ali, alisema ni takribani miaka 20 imefika toka kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, hivyo katika kumuenzi hatoacha kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kupambana na adui ujinga, maradhi na umasikini, pia kuwahamasisha wananchi kulipa kodi ili kuongeza pato la taifa. 

Mkongee alisema kwa kutambua umuhimu wa maji, ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka  2015/20 imeweka lengo la kuhakikisha ifikapo 2020 wananchi wanaoishi vijijini wanapata maji safi na salama kwa asilimia 85.

“Hivyo katika ilani hiyo kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2018 kwa upande wa vijijini miradi 1,659 imekamilishwa, lakini bado Serikali ina sera za kimkakati za uchimbaji wa visima vya maji virefu na vifupi ambavyo  vimegharimu Sh biliono 14,” alisema Mkongee. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles