30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenge kukagua, kuzindua miradi ya bilioni 11 Kisarawe

Na Asha Bani, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amepokea Mwenge wa Uhuru, huku ukitarajiwa kuzindua miradi nane ya maendeleo yenye thamani ya Sh  bilioni 11.67.

Jokate amepokea Mwenge huo leo Jumapili Julai 27, kutoka kwa  Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaibu Nnunduma.

Jokate amesema mwenge utakimbizwa kilomita 153.1 kuzindua miradi nane ikiwamo ya  maji na miundombinu mbalimbali sambamba na kutembelea vituo  vinavyotoa huduma za dawa za kulevya ,rushwa na ugonjwa wa maralia.

“Nimepokea Mwenge huu ukiwa safi kabisa na tutatembe km 153.1 tutazindua miradi pamoja na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali wilayani humu ikiwa ni sambamba na kutembelea vituo mbalimbali vinavyotoa huduma za kijamii,” amesema Jokate.

Amesema  Kisarawe wanakwenda sambamba na kauli mbiu ya ‘Maji  ni haki ya kila mtu tutunze vyanzo na kushiriki uchaguzi serikali za mitaa’ ambapo utunzaji wa maji unazingatiwa pamoja na kuongeza maeneo ya upatikanaji wa maji na kuibua vyanźo vipya vya maji.

“Bila kujali dini ,kabila wala siasa kwamba kila mtu anatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kushiriki shughuli za mwenge huo na kufahamu maendeleo ya wilaya yao.

 Naye Mkuu wa Wilaya Mafia, Nnunduma amesema wamekimbiza kilomita 102 na kukagua miradi nane pia, japo zoezi hilo halikufanikiwa kwa asilimia  100 kwa kuwa kuna miradi miwili ilileta shida kwa sababu gharama zilizotajwa na utekelezwaji wake ulikwenda tofauti kwamba hapakuwa na uwiano.

“Kutokana na hilo kiongozi wa mwenge aliagiza Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), suala hilo ili kufahamu uhalisia wake ukoje,” alimesema Nnunduma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles