24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MWENDOKASI DAR YAINGIZA BIL. 19/-

NA AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM

SIKU moja baada ya Rais, Dk. John Magufuli, kuwabana mawaziri wawili wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene na mwenzake wa Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kutaka wajieleze kuhusu mapato ya mradi wa Mabasi ya Mwendokasi (DART), hatimaye mapato yameanikwa hadharani.

Mradi huo ambao ulianza kutoa huduma jijini Dar es Salaam Mei mwaka jana, hadi sasa umeshakusanya Sh bilioni 19.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri Simbachawene  alisema mradi huo kwa sasa unahudumia abiria wapatao 200,000  na mapato yake yamekuwa yakiongezeka  kila mwezi.

“Tulianza kwa makusanyo ya shilingi milioni 800 kwa mwezi Mei, Julai ikapanda ikaja shilingi bilioni moja kwa mwezi, badaye ikaja shilingi bilioni mbili,” alisema Simbachawene.

Alisema katika miezi miwili ya mwisho Novemba na Desemba makusanyo yalizidi kuongezeka na kufikia Sh bilioni 3 kwa mwezi.

“Biashara hii inaonekana nzuri ingawa lazima tujue coast (gharama) za uendeshaji, maana katika fedha hizo  hapo bado hujatoa mafuta, uendeshaji mishahara na kuna wadau wengi wanaofanya mradi uwepo hayo yote ni masuala ya mahesabu,” alisema Simbachawene.

Alisema katika mchanganuo wa fedha hizo  mpaka sasa msimamizi wa miundombinu hiyo ambao ni DART wanalipwa Sh milioni 8.1 kwa siku.

“Dart wanalipwa chao shilingi milioni  8.1 ya utumiaji miundombinu  kwa siku, kila siku wanapata chao tumeona bora huo mfumo kuliko kuingia kwenye mahesabu,” alisema Simbachawene.

Alisema awali DART ilikuwa ikilipwa Sh milioni 4.4  kabla ya bodi ya usimamizi ya mradi huo kufanya marekebisho baada ya uchunguzi .

“Kwa sasa mradi ule unailipa DART fedha hizo bila kukosa kila siku, inakatwa moja kwa moja kutoka kwenye System (mwezi) ambayo kwa mwezi sawa na shilingi milioni 200, sasa hapo tujiulize, je kwa hizo fedha  wanaweza kujiendesha mishahara na mambo mengine kama umeme,” alisema Simbachawene.

Waziri Simbachawane, alisema mradi huo una wabia wengine ambao wapo kwenye uendeshaji wa mabasi yake ambao ni UDART, mkusanyaji wa mapato Max Malipo, Benki ya NMB ambao ni wawezeshaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles