25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Mwekezaji akamatwa akilima shamba la bangi

Mwandishi Wetu – Kilimanjaro

KIKOSI cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini, kimemkamata raia wa  Poland, Damian Sanikowsiki (40) kwa tuhuma za kulima shamba la bangi eneo la Njiapanda ya Himo, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio jana, Kaimu Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo, James Kaji, alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa juzi Jumamosi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwapo kwa shamba hilo.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamishina Jenerali, mtuhumiwa amekamatwa pamoja na watu wengine na kwamba mahojiano na watuhumiwa yanaendelea ikiwamo kukusanya vielelezo.

“Watanzania wote tujaribu kuangalia kwamba si kila mwekezaji anauwekezaji halali kama ambavyo tumeweza kukuta hapa, kwani ikizingatiwa kwamba kwasasa kuna malumbano makubwa juu ya kutaka kuruhusu kilimo cha bangi kwamba ilimwe kwa ajili ya dawa.

“Lakini nitoe angalizo kwamba ni vyema tujitahidi kutoa elimu ili wananchi waweze kuelewa kwamba sheria inaruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya dawa na dawa hizo siyo mmea wa aina hii iliyokamatwa inaweza kutengeneza dawa hapa kuna mimea maalum,” alisema Kaji.

Aidha, alisema kuwa sheria pia inakataza ulimaji na matumizi mengijne ya bangi ambayo mikoa na wananchi wengi wamekuwa wakijihusisha nacho jambo ambalo linawapa ugumu wao kamamlaka kuruhusu aina hiyo ya kilimo.

 “Hivyo tutakaporuhusu wawekezaji kuanza kulima bangi kwa ajili ya dawa udhibiti wake bado hatujawa tayari, kwnai mfano huyu amekuja kama mwekezaji, hivyo mamlaka inaposema hapana kwa kipindi hiki basi tuweke makubalino hadi tutakapodhibiti kilimo hiki ambacho ni haramu,”

Alisema mamlaka hiyo haiwezi kuwa na mtu kila sehemu na kuweza kuthibiti, na kwamba wanatakiwa kuangalia mtu anapowekeza anaajiri watu wangapi huku akieleza kuwa mtuhumiwa amekuwa ni mtu w arushwa.

“Nyumbani tulimkuta yeye, mke wake ambaye ni Mtanzania mwenezetu, rafiki zake na mtoto mdogo, pia amekuwa ni mtu wa rushwa jambo ambalo hata mamlaka za hapa hazifahamu. Kwani vijana wangu walipokuja kumkamata alitoa ahadi ya kutoa Sh milioni 10 na alizileta pale ili mambo yaishe na kuahidi kuwa waingie mkataba kila mwsiho wa mwezi atakuwa antoa Sh milioni 40,” alisema Kamishna Kaji.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa pia akiwa na bangi iliyoongezewa thamani kwa kuiweka kwenye keki na nyingine iliyosindikwa mfano wa asali ambayo hutumiwa na wateja wa ndani na nje ya Tanzania.

Februari 6, mwaka huu, Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba, aliibua hoja ya kuitaka  Serikali kuruhusu kilimo cha bangi nchini ili wakulima waweze kuchangamkia soko la zao hilo ambalo limepanda kwa kiwango kikubwa duniani kabla halijaporomoka.

Kauli ya, Kishimba iliungwa mkono na Spika wa Bunge Job Ndugai, akisema hicho anachochangia Kishimba sio utani, kwani na yeye hivi karibuni alikuwa Canada kwenye mkutano wa maspika wa nchi za Jumuiya ya Madola Duniani na ameliona hilo.

Alisema bei ya bangi duniani imepanda mara dufu na nchi zote zinazotuzunguka zimesharuhusu kilimo cha bangi.

Alisema waliopiga marufuku bangi ni wazungu miaka ya 1940, lakini wazungu wale wale ndio waliogundua kuwa ndani ya bangi kuna dawa.

Wakati akiendelea na mchango wake, alisimama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki akiomba kutoa taarifa.

Alipopewa nafasi na Spika Ngugai, Kairuki alisema anaiona hoja ya Mheshimiwa Kishimba na tayari wao wizarani wamepata wawekezaji  wawili ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika kilimo na kuchakata mafuta ya bangi kwa ajili ya matibabu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles