Mwasiti awapa neno chipukizi

0
742

Glory Mlay

MSANII wa bongo fleva, Mwasiti Almasi, amewakumbusha vijana wanaotaka kuingia kwenye tasnia ya muziki kuwa kazi hiyo haina  mteremko, ila inahitaji juhudi binafsi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwasiti alisema ili msanii afanikiwe ni lazima ajitume na ajue anachokitaka katika kazi yake hiyo.

“Kuliko vyote lazima ujue unataka nini ndani ya muziki, ni vizuri ukajua kabisa kwamba hii ni biashara na biashara bidhaa zinaweza kuwa zinafanana kwa uso lakini zikawa na ladha tofauti.

“Kama unafanya kazi vizuri na unajua unataka nini hata ushindani wenyewe utakuwa unakupa changamoto za kawaida ambazo unaweza kupambana nazo,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here