27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MWANZA WAJIANDAA KUPATA MBADALA WA MV BUKOBA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

Na BENJAMIN MASESE-MWANZA

SERIKALI imesema imeanza utaratibu wa  kujenga meli kubwa ya kisasa ambayo itakuwa mbadala wa MV Bukoba iliyopata ajali ya kuzama Mei 21, mwaka 1996 na kusababisha zaidi ya watu 800 kupoteza maisha.

Akizungumza wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Mwanza juzi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema tayari Serikali imeanza taratibu za  ununuzi wa meli mpya ya kisasa itakayotoa huduma mkoani Mwanza na Bukoba.

Bila kufafanua kiasi kilichotengwa, Profesa Mbarawa, alisema tayari Serikali imeshatenga fungu kubwa na majadiliano ya ununuzi yataanza Desemba 19, mwaka huu huku akiwataka watumishi kubadilika na kufanya kazi kama Serikali ya awamu ya tano inavyoelekeza.

“Meli tuliyopanga kuinunua itakuwa ya kisasa na uwezo wake ni kuchukua watu 12,000 na tani 400 za mizigo, watu wa Kanda ya Ziwa wana haki ya kupata  chombo hiki  na itakuwa mbadala wa MV Bukoba.

“Tunataka kuimarisha sekta ya usafirishaji ndio maana tunanunua ndege, meli na hivi sasa ujenzi wa reli ya kisasa kwa awamu ya kwanza unaanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, lakini ndani ya miaka mitatu tangu sasa tutakuwa na treni hiyo ambayo itakuwa inatumia saa 11 kutoka Dar hadi Mwanza,” alisema.

Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa alitembelea Barabara ya Usagara – Kisesa yenye urefu wa kilomita 16 huku akisikitishwa na hatua ya ujenzi wake kutokamilika haraka, ambapo alimtaka Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Roads Works kukamilisha na kuikabidhi  ifikapo Februari 15, mwakani.

Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Rubirya, alisema hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa Sh bilioni 6 kati ya Sh bilioni 9.3, hivyo anaidai Serikali bilioni 3.1 huku mkandarasi mshahuri amelipwa Sh bilioni 1.2 na anadai Sh milioni 900.

“Katika ujenzi huu jumla ya Sh milioni 806 zilitengwa kwa ajili ya kulipa fidia ya umiliki wa ardhi, upitishwaji wa barabara kukatisha reli, kuhamisha nguzo za umeme, mabomba na maji na miundombinu mingine, lakini hadi sasa tumetumia Sh milioni 257.2 kulipa fidia,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles