29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

MWANGWI WA JPM WAPANGUA MAKAMANDA WA POLISI MIKOA

Na MWANDISHI WETU,Dar es Salaam


SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kueleza kukerwa na ajali za mara kwa mara, hasa mkoani Mbeya, huku Kamanda wa Polisi katika mkoa huo akiwa achukui hatua, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro, amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana na kusainiwa na Msemaji wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa, ilisema aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna wa Polisi (ACP), Mussa Taibu, amerudishwa makao makuu ya jeshi hilo.

Alisema katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Ulrich Matei, anakwenda kuwa RPC Mkoa wa Mbeya.

Mwingine aliyeguswa na uhamisho, ni SACP Deusdedit Nsimeki, aliyekuwa makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu.

Inaendelea………….. Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles