MWANASIASA ATUPIWA MAYAI AKIFUNGA NDOA BRAZIL

0
573

BRASILIA, BRAZIL


MWANASIASA nchini hapa amewashutumu waandamanaji wa mrengo wa kushoto kwa kuvurumisha mayai kumshambulia pamoja na wageni wakati wa harusi yake.

Waandamanaji hao walifanya kitendo hicho, kuonesha kupinga familia yake kumuunga mkono Rais Michel Temer, ambaye anakabliwa na tuhuma za rushwa.

Mwanasiasa huyo, Maria Victoria Barros (25) ambaye ni mbunge wa Panara, pia ni bintiye Waziri wa Afya Ricardo Barros. Aidha mama yake Cida Barghetti, ni naibu gavana wa Parana

Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya kanisa ambako sherehe hizo za harusi zilikuwa zikifanyika Ijumaa jioni.

Waandamanaji hao walirusha mayai na mwanasiasa huyo akalamizimika kuondoka akitumia gari lisilopenya risasi

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wanasiasa wengi wa taifa hilo akiwamo baba yake Barros na mama yake Cida Barghetti.

Takriban wabunge 30 walialikwa kusafiri kutoka mji mkuu Brasilia kuhudhuria harusi kwenye mji mkuu wa jimbo la Parana Curitiba.

Picha katika mtandao wa You Tube zinaonyesha walinzi wakifungua miavuli kuwakinga bibi na bwana harusi walipokuwa wakiondoka kanisani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here