29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MWANASAYANSI MKONGWE AUSTRALIA KWENDA ‘KUJIUA’ USWISI

SYDNEY, AUSTRALIA


MWANASAYANSI mkongwe zaidi nchini Australia, ambaye alitengeneza vichwa vya habari duniani wakati chuo chake kikuu kilipojaribu kumuondoa ofisi yake alipokuwa na umri wa miaka 102 ataelekea Uswisi mapema mwezi huu ili kuhitimisha maisha yake.

Hatua hiyo imeibua upya mjadala wa kitaifa kuhusu haki ya kusaidiwa kufa.

Mwanasayansi huyo, David Goodall (104) hana ugonjwa mbaya unaohatarisha maisha lakini ubora wa maisha yake umezorota na hivyo ameomba msaada wa shirika linaloendesha huduma ya kujiua mjini Basel, wanaharakati watetezi wa haki ya kusaidiwa kufa walisema.

“Ninasikitika sana kufikia umri huu,” mtaalamu huyo wa jiolojia aliliambia Shirika la Utangazaji la ABC la hapa wakati wa kusherehekea siku yake ya 104 ya kuzaliwa mapema mwezi uliopita.

“Sina furaha. Ninataka kufa. Hili si suala la kuhuzunisha. Huzuni ni pale unapozuiwa kutimiza matakwa yako.

“Hisia yangu ni kwamba mtu mwenye umri mkubwa kama mimi ninapaswa kuwa na haki kamili za kiraia ikiwamo ya kusaidiwa kufa,” aliongeza.

Kusaidiwa kufa ni kosa katika nchi nyingi duniani na kumepigwa marufuku Australia hadi jimbo la Victoria lilipokuwa la kwanza kuhalalisha kitendo hicho mwaka jana.

Lakini sheria hiyo, ambayo itaanza kutumika jimboni humo kuanzia Juni 2019 itahusu wagonjwa,  ambao wana maradhi mabaya, ambao hawatarajii kupona wakiwa na wastani wa kuishi kusikozidi miezi sita.

Majimbo mengine ya Australia yameanzisha mijadala kuhusu kitendo cha kusaidiwa kufa lakini mapendekezo yaliyowasilishwa bungeni yameshindwa kupata kura za kutosha kuungwa mkono.

Jimbo la karibuni zaidi ni New South Wales mwaka jana.

Taasisi ya Exit International, ambayo inamsaidia Goodall kufanikisha safari hiyo, ilisema si haki kwa mmoja wa raia wenye umri mkubwa na mashuhuri Australia kulazimishwa kusafiri kwenda nje kufa kwa amani.

“Kifo cha amani na heshima kinapaswa kuwa haki ya kila mmoja akitakacho. Na watu hawapaswi kulazimishwa kuondoka nyumbani kwenda kukitafuta kwingine,” ilisema katika tovuti yake jana.

Kundi hilo liliendesha kampeni mtandaoni ya kufanikisha upatikanaji wa tiketi ya ndege kwa ajili ya Goodall na msaidizi wake na hadi sasa dola 13,000 sawa na Sh milioni 27 zimkusanywa.

Goodall, mtafiti wa heshima katika Chuo Kikuu cha Edith Cowan mjini Perth aliibuka katika vyombo vya habari vya kimataifa mwaka 2016 wakati alipotangazwa na chuo hicho kuwa hafai kuishi katika kampasi za chuo.

Baada ya kelele na kuungwa mkono na wanasayansi duniani, uamuzi wa kumuondoa ukasitishwa, ambapo aliendelea kuzalisha nyaraka za kitafiti

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles