31.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAMUME AMCHINJA MKEWE, AJINYONGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Andrew Satta
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Andrew Satta

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MWANAMUME mmoja ambaye jina lake halikupatikana amemuua kwa kumchinja mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake ambaye naye jina lake halikufahamika.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika maeneo ya Tandika, Davis Corner ambako mwanamume huyo alimchinja mwanamke huyo kwa kutumia sime na kisha yeye mwenyewe kujinyonga kwa kutumia mkanda wa begi.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Andrew Satta, alisema tukio hilo linatokana na wivu wa mapenzi na lilimuhusisha mwanamume huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 47 huku mpenzi wake akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 33.

“Kijana huyo alimchinja mpenzi wake kwa wivu wa mapenzi baada ya kuhisi ana uhusiano na mtu mwingine, baada ya kupishana Kiswahili katika maongezi ndipo aliamua kumchinja kwa sime na kusogea mita 60 mbele na yeye kuamua  kujinyonga kwa kutumia mkanda wa begi. Watu hao wote majina yao bado hatujayafahamu,” alisema Satta.

Alisema mwanamke aliyeuawa ameacha watoto wawili ambao ni mapacha wenye umri wa miaka mitatu.

Satta alisema maiti zote zimehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke wakati jeshi hilo likiendelea na uchunguzi wa mauaji hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles