24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanamke azinduka baada ya kupoteza fahamu miaka 27

MWANAMKE  mmoja kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambaye aliumia vibaya katika ajali ya gari iliyotokea mwaka 1991 na kupoteza fahamu amewastaajabisha wengi baada ya kuamka ikiwa ni miaka 27 tangu apoteze fahamu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari jana, mwanamke huyo, Munira Abdulla, alipata ajali hiyo ya kugongwa na basi akiwa na umri wa miaka 32 na kupata jeraha katika ubongo wakati akiwa anakwenda kumchukua mtoto wake shule.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mtoto wake Omar Webair, alikuwa na umri wa miaka minne wakati yeye na mama yake walipopata ajali.

Hata hivyo, mtoto huyo ambaye alikuwa ameketi kiti cha nyuma hakujeruhiwa hata kidogo na alikutwa akiwa amekumbatiwa na mama yake.

Maendeleo hayo mazuri ya afya yake yalianza mwaka jana alipohamishiwa katika hospital moja nchini Ujerumani.

mtoto wake, Omar ameweka wazi kuhusu ajali waliyoipata na kuelezea utaratibu wa matibabu ya mama yake yaliyochukua miaka mingi.

“Sikuwahi kukata tamaa kwa sababu kila siku nilihisi kuwa kuna siku mama yangu ataweza kuamka” alisema Omar.

Omar alisema kuwa kuna sababu kubwa ambayo imemfanya asimulie mkasa uliomkuta mama yangu akidai ni kutaka kuwaambia watu kuacha kukata tamaa kwa watu wanaowapenda na mtu akifikia hatua hiyo haimaanishi kuwa amekufa.

Kijana huyo alisema kuwa mama mkwe wa Munira ndiye alikuwa dereva  na kwamba mama yake  alikuwa amekaa naye katika kiti cha nyuma, na alipoona wanakaribia kupata ajali, alimkumbatia ili kumuokoa.

Alisema kuwa katika ajali hiyo  hakuumia bali alibaki na jeraha dogo kichwani lakini mama yake ambaye aliumia alichelewa kupata matibabu kwa saa kadhaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles