32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mwanamke aliyeolewa na paka kuepuka migogoro ya ndoa

mmh

DUNIA haiishi vituko siku hadi siku, kama kisa cha mwanamke huyu raia wa Uingereza, Barbarella Buchner alivyotoa kali ya mwaka baada ya kufunga ndoa na paka wake wawili mwaka 2004, ambayo aliidhinisha miaka 10 mapema mwaka jana.

Akizungumzia tukio hilo lisilo la kawaida, mwanamke huyo anasema alichukua uamuzi huo baada ya kuona hatoweza kuolewa na mpenzi yeyote yule wa kiume kufuatia kukorofishana na kisha kuachika na wapenzi wake saba.

Wakati Barbarella Buchner alipotengana na mpenzi wake wa kiume wa saba na wa mwisho, aliingiwa na wazo kwamba hatapata mpenzi mwingine tena.

Lakini kwa mawazo yake aliona kwamba kwanini asihamishe mapenzi kwa marafiki na ndugu zake wakubwa na waaminifu ambao muda wote wapo mbele yake, paka wake wawili.

Barbarella akaamua kufunga ndoa na paka hao wa kiume waitwao Spider na Lugosi na waliadhimisha miaka 10 ya ndoa yao Januari mwaka jana.

Alienda mbali kwa kuweka tattoo za herufi za kwanza za majina yao katika mguu wake wa kulia, akisema paka hao ni wapenzi wa maisha yake yote.

“Kabla nilikuwa na uhusiano na mwanadamu, huja nyumbani na kugombana kuhusu hiki na kile na atataka tuzungumze wakati mimi sijisikii na kadhalika.

“Lugosi na Spider ni tofauti – ninaishi nao kwa furaha. Siko mpweke, nina paka wangu sasa. Sijutii chochote na sijali kile watu wasemacho.”

Barbarella mwenye umri wa miaka 49, ambaye kazi yake ni ubunifu wa tovuti kwenye mtandao wa intaneti ameongeza kuwa “Kuna baadhi ya wanawake wamepangiwa kufanya usafi kwa ajili ya waume zao na wameridhia kufanya hivyo, kwangu ni tofauti.”

Kwangu nimetua mzigo huo, sioni shida kuwa na waume wangu paka na nitahakikisha wanaishi kwa furaha kama ndoa inavyohitaji.

Kuhusu mapemzi yake na paka jinsi yalivyoanza, anasema: “Nikiwa mdogo, daima zilizungukwa na paka – familia yetu ilimiliki paka mmoja au wawili.”

“Sikumbuki lini sikuwahi kuwapenda paka au wanyama kwa ujumla. Lakini paka ndiyo chaguo namba moja kwangu.”

Hata hivyo, Barbarella kamwe hakuridhishwa na uhusiano wake na paka wa familia yao na hivyo alitamani siku moja kuwa na paka wake mwenyewe.

Anaeleza: “Paka hao hawakuwahi kuwa wangu. Waliasiliwa na wazazi wangu. Sikuweza kuwa na uhusiano nilioutaka kwa sababu sikuwalisha paka wa familia. Wazazi wangu ndio waliowalisha.

“Lakini, wazazi wangu walinifundisha tangu miaka ya awali kuwaheshimu paka na kutokuwa mbaya kwao.”

Wakati Barbarella mwishowe alipopata fursa ya kuasili paka wake mwenyewe akiwa na umri wa miaka 34, aliichukulia uzito fursa hiyo.

Anasema: “Kwangu ilikuwa kana kwamba pale unapogundua unapata mtoto. Kabla ya kupata mtoto au kumuasili, unazama katika intaneti kujifunza kwa kadiri unavyoweza.

“Unasoma vitabu vingi na kuhudhuria makundi ya kijamii na hili ndilo nililofanya kabla ya kuasili paka hawa,” anasema.

Machi 2000, Barbarella aliasili rasmi paka wenye umri wa miezi saba kutoka makazi ya wanyama mashariki mwa London.

Anasema lilikuwa penzi kali wakati nilipowatupia macho wavulana wangu wawili, Lugosi na Spider kwa mara ya kwanza. Hakika sitaisahau siku hiyo.

Barbarella – ambaye kwa sasa anaishi Lanzarote, Hispania amekuwa na uhusiano wa muda mrefu na wanaume lakini kamwe hawakumuoa na lilimfanya akate tamaa hasa baada ya kuachana na mwanamume na yule wa mwisho.

“Iliniuma mno kuachana naye. Nililia mno kwa wiki kadhaa baada ya kutengana. Lakini paka hawa walinisaidia kupita kipindi hicho kigumu.”

“Nilikuwa nikilia nikiwa nimewaegemea Lugosi na Spider. Walikuwa katika sofa pamoja nami hakika walinifariji mno kipindi hicho.”

Ni kwa sababu hiyo niliiamua mwaka 2004 kufunga ndoa nao kupitia mtandao unaoendesha shughuli hizo ujulikanao kama marryyourpet.com.

Baada ya kukubaliwa na wanawake wawili wanaoendesha tovuti hiyo na kulipa ada Barbarella alifunga ndoa na Lugosi na Spider katika sherehe iliyofanyika Januari 9 mwaka huo na kupatiwa cheti cha ndoa kuhalalisha ndoa yao hiyo.

Mwaka huo huo, Barbarella alihamia Lanzarote na paka wake hao kuanza kuishi maisha mapya ya ndoa.

Kuhusu kufanya tendo la ndoa na paka, anasema hicho si kitu kilicho akilini mwake bali mapenzi ya kupendana kutoka moyoni yasiyo bila kuhusisha tendo la ndoa.

“Iwapo ninatongozwa na wanaume, huwaambia moja kwa moja kwa kuwatazama usoni, ‘nimeolewa na paka wangu.”

Anasema maisha ya ndoa paka wake ni rahisi. “Kwa kadiri nilivyokuwa na mpenzi wangu kwa miaka michache ya kwanza, akaanza kuwa mvivu.

“Nilirudi nyumbani na kukuta nguo zake zimetapakaa sakafuni sebuleni. Daima nilizikusanya.

“Uhusiano wangu na Lugosi na Spider ni tofauti kwa sababu ninakubali wao ni paka. Hawawezi kunipekleka hospitali ninapoumwa na hawaweza kuniandalia chakula. Wao ni kampani yangu tu,” anasema.

Anasema kutokana na mapenzi makubwa kwa paka wake hao yuko tayari kufilisika ili mradi paka wake wale vizuri, wahisi vizuri na kwa afya akikumbushia kwamba vyakula vyao ni ghali kuliko chake.

Anasema yuko tayari kuua ili kuwalinda paka wake, akisema bora aende jela ili paka wake waendelee kuishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles