22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

 Mwanamke akutwa na bunduki 3, majambia

Leonard PauloNA OSCAR ASSENGA, KILINDI

JESHI la Polisi mkoani Tanga limemkamata mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Kimamba, Kata ya Negero  wilayani Kilindi, Tabu Chabai (23) kwa tuhuma za kushirikiana na mtandao wa majambazi.

Vilevile, mtuhumiwa mwingine, Waziri Luhaya, anatafutwa na jeshi hilo kuhusiana na tukio hilo, baada ya kutoroka.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo, alisema Chabai alikamatwa Mei 2, mwaka huu  usiku katika Kijiji cha Kimamba, Kata ya Negero.

Kwa mujibu wa Kamanda Paul, mtuhumiwa huyo alikamatwa    polisi walipokuwa kwenye msako maalum wa wahalifu.

“Kuna taarifa kutoka kwa raia wema zilitufikia na tukaamua kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa huyo kufanya upekuzi na kukuta vitu mbalimbali
vilivyokuwa vikitumika kwenye uhalifu.

“Mtuhumiwa huyo alikutwa na silaha mbalimbali zikiwamo bunduki tatu za shortgun zilizotengenezwa kienyeji, bastola moja iliyotengenezwa kienyeji, risasi za shortgun 51 na ganda moja la risasi.

“Tulikamata pia panga moja, majambia mawili, simu 14 za aina mbalimbali, makoti matatu, kofia za kininja na shati linalodhaniwa kuwa ni la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Vitu hivyo, vilikamatwa vikiwa vimehifadhiwa kwenye mfuko wa sulphate,” alisema Kamanda Paulo.

Kamanda  alisema polisi  wanaendelea kuwashikilia watu saba kuhusiana na matukio ya uhalifu kabla hatua za  sheria hazijachukuliwa dhidi yao.

“Kwa hiyo, nawaomba wananchi tuendelee kushirikiana   kuhakikisha tunawafichua wahalifu ili maeneo yetu yaendelea kuwa salama,” alisema.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Tanga, limekamata kilo 802 za mirugi iliyokuwa ikisafirishwa kutoka   Kenya kwenda  Dar es Salaam.

Kamanda Paulo alisema  jana kwamba mirungi hiyo ilikamatwa katika Kijiji cha Mtimbwani, Kata ya Mtimbwani wilayani Mkinga, polisi walipokuwa kwenye operesheni ya kukabiliana na wahalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles