Mwanamke aangua vifaranga vya bata

0
785

WASHINGTON, Marekani

MWANAMKE mmoja ameangua bata watatu na kuwapa majina ya Beep, Peep na Meep kwa kutumia mayai aliyonunua kutoka duka moja la kufanya manunuzi.

Charli Lello mwenye umri wa miaka 29 kutoka Hertfordshire, aliweka mayai hayo kwenye kiangulio ili kupitisha muda wakati ambapo walihitajika kusalia nyumbani kwasababu ya virusi vya corona.

Alisema bata hao watakuwa na maisha mazuri kwa pamoja na kuku wake wadogo.

Msemaji wa duka hilo, alisema mayai ambayo yanaweza kuangua ni salama kwa matumizi na hayawezi kutofautishwa na mayai ya kawaida, labda tu yawekwe kwenye kiangulio.

Lello ambaye kawaida anafanya kazi kama naibu meneja katika duka hilo, alipata wazo baada ya kuona video ikisambaa kwenye mtandao wa Facebook iliyomuonesha mtu mmoja akiangua mayai ya kware aliyonunua kutoka kwa duka kubwa la manunuzi.

“Nilipokuwa katika duka la Waitrose, niliona mayai ya bata nikaanza kufikiria yanaweza kufanya vizuri pia. Nilikuwa na hamu sana ya mayai haya kuangua lakini pia nilifahamu fika kwamba nimeyanunua dukani.

“Yamechukuliwa, yakatingishwa yakiwa kwenye gari la kuyasafirisha, kisha yakazungushwa yakiwa kwenye toroli wakati yanasubiri kupangwa kwenye rafu za dukani, pia hakuna anayeweza kusema yameokotwa na kurejeshwa na watu wangapi, kwahiyo nilijua kwamba yanaweza yasiangue.”

Mwezi mmoja baada ya kuyaweka kwenye kiangulio, Lello, alisikia sauti kwa mbali na baadae vifaranga vikaanza kujitokeza kutoka kwenye ganda la yai.

Alisema hiyo imekuwa tajriba nzuri kuona mayai ya dukani yakiangua vifaranga lakini hicho ni kitu ambacho hatakirudia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here