29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

MWANAKIJIJI AMUUA MKEWE, AJINYONGA

MOROGORO NA LILIAN JUSTICE


WATU watatu wamefariki dunia mkoani Morogoro katika maeneo tofauti ikiwamo mwanaume kumuua mkewe kwa kutumia kitu  chenye ncha kali kichwani  kabla ya  kujinyonga na mwingine  kuuawa kwa kupigwa kichwani  na usoni na kitu butu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mtafungwa  alisema    tukio la kwanza lilitokea   Julai 28 mwaka huu   asubuhi   katika eneo la Njage Tarafa ya Mngeta wilayani Kilombero.

Alisema    Rose Mngwe (43)  mkazi wa Njage aliuawa na mumewe,  Jacob Kambo kwa  kukatwa na shoka  kichwani  kabla ya mumewe huyo kujinyonga kwenye mti kwa kutumia kamba .

Ilielezwa  chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa  familia  na tayari miili ya wanandoa hao imekwisha kufanyiwa uchunguzi  kwa ajili ya kufanya utaratibu wa mazishi.

Tukio la pili lilitokea  ulai 30 mwaka huu   alfajiri  maeneo ya Kitongoji cha Igagafu  Kijiji cha Msowero  wilayani Kilosa ambako  mzee Leo  Charles ( 61) mkazi wa Igagafu aliuawa  kwa kupigwa na kitu butu   kichwani na usoni na mwanae,   Emanuel Charles.

Kamanda Mtafungwa alisema  mtuhumiwa alikamatwa   na atafikishwa mahakamani  uchunguzi utakapokamilika.

Alitoa wito kwa wananchi  kuacha kujichukulia sheria mkononi na   kuepuka msongo wa mawazo  unaosababisha  kujidhuru.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles