28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

MWANAJESHI JORDAN ALIYEUA WASICHANA AACHIWA HURU

TEL AVIV, Israel


MWANAJESHI wa Jordan ambaye aliwaua wasichana saba wa shule  nchini Israel ameachilia baada ya kutumikia  kifungo cha miaka 20 gerezani.  

  Ahmed Daqamseh alihukumiwa kufungwa kwa kuwafyatulia risasi wasichana wa Israel wakiwa  katika kisiwa kilicho karibu na mpaka na Jordan.

Mahakama ya jeshi ilimtaja Daqamseh kuwa alikuwa na matatizo ya akili wakati anafanya hivyo  na kumhukumu kifungo cha maisha jela.

Aliyekuwa mfalme wa Jordan aliomba msamaha kwa suala hilo na kutembelea familia za wasichana hao nchini Israeli kutoa rambi rambi zake na kulipa fidia.

Israel haijasema lolote kuhusu kuachiliwa kwa mwanajeshi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles