Mwanajeshi Gambia akiri kuua kwa agizo la Rais

0
709

Banjul, GAMBIA

Mwanajeshi mmoja nchini Gambia, Luteni Malick Jatta, amekiri kuua watu 50 mwaka 2005 kwa agizo la aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kwa hofu ya kupinduliwa na watu hao.

Luteni Jatta amesema hayo wakati akitoa ushahidi wa mauaji ya wahamiaji yaliyotokea nchini humo mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRRC), inayochunguza maovu yaliyotekelezwa chini ya utawala wa miaka 22 ya Jammeh.

Mwanajeshi huyo wa zamani awali alikiri pia kuhusika  katika mauaji ya mwandishi wa habari na mhariri wa gazeti la The Point, Deyda Hydara mwaka 2004 kwa agizo la Jamme ambapo alilipwa Dola za Marekani 1, 000 kutekeleza tukio hilo.

Jamme ambaye anaishi uhamishoni nchini Guinea ya Ikweta ambako alikimbilia mwaka 2017 baada ya kushindwa uchaguzi alikana kuhusika katika kifo cha mwanahabari huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here