Uturuki
Mahakama nchini Uturuki imewahukumu wanajeshi 32 wa zamani, kifungo cha maisha jela kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi mwaka 2016 lililopangwa kumuondoa madarakani Rais Recep Tayip Erdogan.
Kesi dhidi ya kikosi hicho ilianza kusikilizwa mnamo mwezi oktoba mwaka 2017 huku hukumu ya wanajeshi hao 32 ilitolewa katika chumba maalumu kilichojengwa kwaajili ya kusikilizwa kesi za majaribio ya kimapinduzi  katika gereza la Sincan mkoani Ankara.
Pia nchi ya Uturuki inamtuhumu shekhe wa dini ya kiislamu anayeishi uhamishoni, Fethullah Gulen kwa kupanga jaribio la mapinduzi ya mwaka 2016.
Jaribio la mapinduzi lilisababisha vifo vya watu 248 mbali na wanajeshi waliohusika na jaribio la mapinduzi waliouliwa usiku wa tukio.