24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanahabari Shermax Ngahemela afariki dunia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwanahabari mkongwe, Shermax Shabaan Ngahemela amefariki dunia jana Desemba 4, 2022 jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali kutoka kwa mtoto wa marehemu, Adam Shermax zimeeleza kuwa maziko yatafanyika leo Jumatatu saa 10 jioni katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Enzi za uhai wake marehemu Shermax amefanyakazi katika kampuni ya New Habari (2006) akihudumu kama Mhariri wa Uchumi na Biashara wa magazeti ya The African na Mtanzania.

Akizungumzia msiba huo mmoja kati ya watu wa karibu waliofanya kazi na marehemu Shermax, Jimmy Charles amesema ni msiba mzito kwa tasnia ya Habari na kwa familia yake.

“Binafsi namfahamu Ngahemera kama rafiki, kaka, mwalimu na mwanahabari aliyeijua kazi yake vizuri. Mwendo ameumaliza,
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi…Amin,” ameeleza Charles.

Mtanzania Digital inatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles