29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi wa kiume anayepata ‘hedhi’

George Fellowes na rafiki yake Amber May Ellis (2)BERKSHIRE, UINGEREZA

KIJANA mmoja wa kiume anayesoma kwenye chuo Kikuu cha Reading kilichopo kwenye mji wa Berkshire huko uingereza, ameushangaza ulimwengu baada ya kudai kuwa hata yeye hupatwa na hedhi anayoiita ‘hedhi ya kiume’.

Mwanafunzi huyo anayeitwa George Fellowes mwenye miaka 22, anasema mara nyingi rafiki yake wa karibu, Amber May Ellis anapokuwa kwenye siku zake na yeye hupata uchungu wa hedhi kila mwezi.

Uchungu huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa, kwenye mahojiano na Newsbeat, George amesema kuwa, “Nadhani ni jambo la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa,” amesema.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile zinazowapata wanawake.

Alisema huwa anapata uchungu chini ya tumbo lake na katika kinena na kwamba huwa anajihisi vibaya na anakuwa mwenye hasira kwa marafiki zake na hisia za mhemuka huwa juu.

“Huwa sipendi kulia wakati huo lakini huwa na hasira nyingi, kuna kitu kimoja kinacho muathiri George hata hivyo sidhani kwamba wanaume wanaweza kupata hedhi bila kutokwa na damu. Wakati unapokuwa na rafiki wa karibu na mtu nadhani homoni zenu hufanana”.

Fellowes anaelezea kwamba wakati alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliyopita alitaka ushauri wa daktari wake. Lakini hakukuwa na maelezo hivyo basi alipewa dawa za kumaliza maumivu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles