22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

MWANAFUNZI MTANZANIA AUAWA AFRIKA KUSINI

NA MWANDISHI WETU

MWANAFUNZI wa shahada ya uzamivu (PhD), Baraka Nafari, aliyekuwa akisoma nchini Afrika Kusini, ameuawa kwa kugongwa na gari na watu wasiojulikana katika kile kinachoelezwa ni mwendelezo wa mauaji ya watu weusi wasio wa taifa hilo.

Mwanafunzi huo ambaye alikuwa akisoma masuala ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) nchini humo, aliuawa Februari 23, mwaka huu na watu wawili waliokuwa wakimfuatilia nyuma na gari.

Uongozi na wanafunzi wanadai tukio la mauaji ya mwanafunzi huyo linahusisha vitendo vya Xenophobia ambapo wahusika walikuwa wanatafuta kupora fedha.

Binamu wa marehemu, Uwezo Gwaliye, anayeishi katika Jiji la Cape Town, jana aliliambia gazeti hili kwamba

mazingira ya mauaji yametokana na ushahidi wa video (CCTV) wa siku ya tukio katika eneo alipokuwa ndugu yake huyo siku ya tukio alikuwa na rafiki yake wakitokea baa wakirudi nyumbani.

Alisema video ya CCTV,  inaonesha Nafari na mwenzake walikuwa wanafuatiliwa nyuma na teksi ambayo ilikuwa na watu wawili ndani yake.

“Awali watu hao walimvaa Nafari lakini alifanikiwa kutoroka kwenda upande wa pili wa barabara ambapo walimfuata na gari wakamgonga na kumbamiza kwenye ukuta wa chuo,” alisema Gwaliye.

Hata hivyo, alisema watuhumiwa wa mauaji hao walikamatwa na kuachiwa baadaye.

Kwa upande mwingine alisema walitoa taarifa katika ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ambao umesaidia kufanikisha mchakato wa kufuatilia tukio hilo.

“Balozi alikuja na kufuatilia mwenendo wa tukio hadi polisi, amewezesha upatikanaji cheti cha kifo cha marehemu. Kwa sasa tunaomba tu mwili uweze kutoka, nadhani Jumatatu ijayo kutakuwa na ibada ya kuaga mwili katika chuo kabla ya kuusafirisha kwenda Dar es Saalam na baadaye Kasulu, Kigoma kwa mazishi.”

Taarifa ya chuo hicho ilisema: “Pamoja na ukweli wa ushahidi wa video, dereva wa teksi alikamatwa kwa kuendesha gari bila leseni kisha aliachiliwa kwa dhamana ya polisi na mtu mwingine katika teksi aliachiwa bila kushtakiwa.”

Aidha, taarifa ya chuo hicho inahoji na kuibua maswali ya mazingira kifo cha mwanafunzi huyo kuwa kwanini walinzi wa chuo na kituo cha Brixton kudhani kuwa mwili wa marehemu ulikuwa wa ombaomba.

Inadaiwa kuwa walinzi wa chuo hawakuhimiza polisi kukagua picha za CCTV mapema hadi ilipofika Februari 28 ndipo Ubalozi wa Tanzania uliweka msukumo na video hizo kuangaliwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles