22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Mwanafunzi aliyepotea akutwa amefariki dunia

JANETH MUSHI -ARUSHA

MWANAFUNZI wa awali katika Shule ya Msingi Themi iliyopo jijini Arusha, Nadia Said (6), amekutwa amefariki, baada ya kupotea kwa muda wa siku mbili.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni, ilieleza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa jana Julai 13, saa mbili asubuhi katika eneo la Old Polisi Line, Themi.

Alisema mwanafunzi huyo aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Jamhuri, alikuwa akiwa amefariki katika shamba la mahindi huku mwili wake ukiwa umelala chali.

Alisema wazazi wa marehemu walidai mtoto huyo alipotea siku ya jumamosi jioni, Julai 11 na walianza juhudi za kumtafuta kwa kutoa taarifa sehemu mbalimbali.

“Aidha uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hili mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa daktari.

“Tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu katima kipindi hiki ambapo jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola tunaendelea na uchunguzi. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhusika na tukio hili,” alisema Hamduni

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles