25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Mwanafunzi afariki dunia akifua mtoni

Gurian Adolf – Sumbawanga

MWANAFUNZI wa darasa la tatu Shule ya Msingi Kianda Igonda wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, Jenifer Kipeta(13)  amekufa maji katika Mto Kianda akiwa anafua sare za shule.

Akizungumzia tukio hilo jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo alisema kuwa tukio hilo lilitoke mwishoni wa wiki ambapo mwanafunzi huyo alikuwa amekwenda kufua sare za shule kwa ajili ya kuzivaa kwa siku ya Jumatatu.

Alisema baada mwanafunzi huyo kufika mtoni na kuanza kufua nguo hizo, ghafla kulitokea maporomoko ya maji na kukawa na mafuriko makubwa ambayo yalimsomba.

Chanzo cha maporomoko hayo ya ghafla yalitokana na mvua kubwa iliyonyesha katika vijiji vya mbali na Kijiji cha Kaianda Igonda ambayo yalisababisha madhara mbalimbali kijijini hapo ikiwepo kifo cha mwanafunzi huyo

Alisema baada ya uchunguzi huo familia ya mwanafunzi huyo ilikabidhiwa mwili kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Kutokana na hali hiyo Kamanda Masejo, alitoa wito kwa wananchi hasa wazazi kuhakikisha wanawalinda watoto ili wawe kwenye mazingira salama wakati wote.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles