27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi afariki dunia akidaiwa kula chakula chenye sumu kwenye sherehe

Na BENJAMIN MASESE – SENGEREMA

MWANAFUNZI wa darasa la saba Shule ya Msingi Mwangika, Mboni Mahano (13) amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Kituo cha Afya Mwangika, baada ya kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu kwenye sherehe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema mwanafunzi huyo anadaiwa kula chakula cha sumu wakati wa sherehe iliyofanyika Agosti 22, mwaka huu  kwa Dorica Omajigo.

Muliro alisema Agosti 23, mwaka huu, baadhi ya  wanawake  waliokuwa na watoto walirejea kwa Omajigo kusafisha vyombo na kula chakula kingine kilichokuwa kimebaki, baada ya saa kadhaa walianza kulalamika kuumwa  tumbo na kukimbizwa Kituo cha Afya Mwangika, lakini mwanafunzi huyo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

“Walioanza kulalamika ni watu wazima wanne, watoto 14 wote walikimbizwa hospitalini na kulazwa, mpaka sasa wanaendelea kupatiwa matibabu, mwili wa marehemu umehifadhiwa hapo na Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafuatilia kwa karibu tukio hili, halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kuhusika na kitendo hiki cha kuweka sumu kwenye chakula,” alisema Muliro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles