24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mwambusi kutimkia Prisons

mwambutsi-jumaNa MWANDISHI WETU- MBEYA

KOCHA msaidizi wa timu ya Yanga, Juma Mwambusi, huenda akajiunga na kikosi cha maafande wa Tanzania Prisons kufuatia mabadiliko yanayotarajiwa kufanyika ndani ya benchi la ufundi la Wanajangwani hao.

Mwambusi alijiunga na kikosi cha Yanga msimu uliopita akitoka katika klabu ya Mbeya City kurithi mikoba ya Charles Mkwasa ambaye alikabidhiwa majukumu ya kuifundisha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Hata hivyo, jana Mwambusi alisimama katika benchi la ufundi la Yanga wakati ikichuana vikali na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa sasa wapo katika mazungumzo na kocha Mzambia, George Lwandamina ambaye anainoa timu ya Zesco, ili aweze kurithi mikoba ya Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi, ambaye inadaiwa atapewa majukumu ya Mkurugenzi wa Ufundi.

Inadaiwa kuwa Mwambusi akiondolewa Yanga upo uwezekano mkubwa wa kurejeshwa kwa Mkwasa ambaye alikubalika sana kutokana na ushauri mzuri aliokuwa akiutoa kwa Pluijm.

Kwa sasa Prisons inafundishwa na kocha Abdul Mingange baada ya Salum Mayanga, aliyeinoa timu hiyo msimu uliopita kutimkia Mtibwa Sugar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles