22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mwaluko ataka mradi wa Shule Bora kutoa mafunzo kwa walimu Singida

Na Seif Takaza, Manyoni

KATIBU Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko ameuagiza Mradi wa Shule Bora kutengeneza mfumo wa kutoa mafunzo kwa walimu wa mkoani humo ili kuinua kiwango cha elimu katika Mkoa huo.

Mwaluko ametoa agizo hilo katika ufunguzuzi wa mkutano wa siku moja ambao umefanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Ikumbukwe kuwa mradi huo wa Shule bora umelenga mikoa tisa ya Tanzania.

Amesema katika uhamasishaji wa Programu ya Shule Bora unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza ukishirikiana na Serikali yaTanzania kwa usimamizi na wahariri wa vyombo vya habari, ambapo walimu watakaopewa mafunzo hayo nao watakwenda kuwafundisha walimu wenzao.

“Ili Progamu hii iweze kufanikiwa Halmashauri zote za Mkoa huu ziwe na waalimu ambapo katika mafunzo hayo yatawagusa walimu wengi kwa wakati mmoja na mpango huu ili ulete tija,” amesema Mwaluko.

Mradi wa Shule Bora umelenga kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za Serikali zilizopo katika mikoa ya  Singida, Dodoma, Simiyu, Tanga, Mara, Rukwa, Katavi, Pwani na mkoa wa Kigoma.
Halikadhalika Katbu Tawala huyo aliwahimiza waandishi wa Habari wa Mkoa huo kuwa Wazalendo katika kuandika Habari za Mkuo huu ili kuutangaza Mkoa katika shughuli za Maendeleo na vivutio vilivyopo Mkoa wa Singida .

“Nashangaa leo hii kuwaona waandishi wa Habari wengi hivi nawaombeni kwa kutumia taaluma yenu mwaka huu Mkoa wa Singida unafikisha miaka sitini hivyo nawaomba mchukue fursa hii kuandika Habari za Mkoa huu tangu uanzishwe Oktoba 15 1963,”amesema Mwaluko.

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka Programu  hiyo kwenye Mkutano wa uhamasishaji wa programu ya shule bora kwa wasimamizi na wahariri wa vyombo vya habari mkoani hapa, Raymond Kanyambo amesema shule bora inabaini changamoto zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa watoto elimu ya awali na msingi na kuzitafutia ufumbuzi ili kila mtoto nchini anapata elimu bora.

Kanyambo amesema kwenye program hiyo kundi la waandishi wa habari litakuwa msaada mkubwa endapo litashirikiana na shule bora kuzibaini changamoto ambazo programu hiyo ikaona umuhimu wa kushirikisha vyombo vya habari ili viweze kusaidia kuhamasisha kuzielewa changamoto zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa watoto shuleni hivyo akatoa wito kwa vyombo vya Habari kuwa Pamoja na Programu hiyo katika kuboresha Ubora wa elimu.

“Tunaomba mshiriki katika programu hii ili tuweze kuzibaini baadhi ya changamoto zinazosababisha watoto wasipate elimu bora hatimaye tutafute njia bora ya kuondoa changamoto hiyo, nina uhakika ninyi waandishi wa Habari mna uwezo wa kuhoji hali ya uandikishaji wa wanafunzi wangapi wameripoti, wangapi wamefaulu, na kama kundi la wenye ulemavu lipo vipi kitaluuma?, hivyo mshirikiane na sisi katika kuinua  elimu kwa watoto wetu,” amesema Kanyambo.

Naye Mwandishi wa Habari Mkongwe, Seif Takaza kutoka Wilaya ya Iramba amemuhakishia Katibu Tawala kwa kutoa ahadi kwamba Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Singida watashirikiana na Programu ya Shule bora ili kuinua kiwango cha elimu mkoani Singida.

“Kwanza natoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya waandishi wenzangu kwamba maagizo yote uliotupa tutayafanyia kazi, tunakuahidi kwamba tutafanya kazi hii ya Mradi wa Programu ya Shule bora tutaifanya vizuri na kwa weledi na taaluma yetu na kuandika habari ya miaka sitini ya Mkoa wetu tatashirikiana kwa pamoja,”amesema Takaza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles