27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu mbaroni kwa kuingiza mamluki kufanya mtihani darasa la saba

 MOHAME HAMAD– MANYARA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, inamshikilia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Orkitikiti, Kijiji cha Engong’ongare wilayani humo, Oscar Waluye kwa tuhuma ya kufanya udanganyifu katika mtihani wa darasa la saba uliomalizika jana nchini.

Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Kiteto, Holle Makungu, alisema mtuhumiwa huyo aliwalazimisha wanafunzi wawili wa darasa la sita katika shule hiyo kufanya mtihani huo, badala ya watahiniwa ambao uwezo wao darasani unaelezwa kuwa ni wa kiwango cha chini.

Alisema mwalimu huyo pia anatuhumiwa kukaririsha mwanafunzi mmoja pamoja na mwanafunzi aliyehitimu shule mwaka jana kufanya mtihani huo. 

Kamanda Makungu alisema baada ya kupata taarifa hizo, walifika shuleni hapo na kuwakuta wanafunzi hao wakiwa wameshafanya mitihani ya masomo ya Kiswahili na Hesabu kinyume na sheria.

“Wanafunzi hao walikuwa wanafanya mtihani huo kwa niaba ya wenzao wa darasa la saba ambao wanadaiwa kuwa na uwezo mdogo huku aliyekaririshwa akitumia jina la mwanafunzi mtoro hapo shuleni,” alidai Kamanda Makungu.

Alisema uchunguzi unaendelea na utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

Alitoa wito kwa walimu kufanya kazi kwa uadilifu kulea watoto katika njia ipasayo ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii badala ya kufanya udanganyifu katika mitihani.

Alisema Takukuru hawatomwonea haya mtu yeyote atakayekiuka sheria za nchi kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu na pia linatengenezwa kundi la wasiojua kusoma na kuandika ingawa wataonekana walifaulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles